BAADHI ya Mitambo ihusikanayo na uchimbaji madini ya Dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold MineLtd,uliopo Kata ya Kakola wilayani Kahama. |
KAMPUNI ya African
Barrick Gold Mines Ltd inayofanya shughuli za uchimbji wa dhahabu katika Mgodi
wa Bulyanhulu wilayani Kahama imeimarisha mahusiano yake na wananchi wa Kata ya
Bulyanhulu ambayo awali yalikuwa
yametetereka na kuzua mgogoro wa mara kwa mara kati yake na jamii
inayowazunguka.
Hali hiyo ilielezwa juzi
Ofisini mwake na Afisa Mtendaji wa kata hiyo;Ramadhani Madese,ambapo alidai hali ya sasa hivi ni shwari kutokana na
idara ya mahusiano ya mgodi huo kukaa na wananchi kwa maelewano jinsi ya
kumaliza kero zinazojitokeza.
Hata hivyo Madese
alikiri kuwa hapo awali idara ya mahusino ilikuwa na mapungufu makubwa kutokana
na maamuzi yake kuyafanya kibabe hali iliyozua migogoro ya mara kwa mara na
wananchi ambao wakati mwingine walikuwa wakiziba barabara kuzuia magari na shughuli
za mgodi zisifanyike.
Kufuatia hali hiyo idara
hiyo ya mahusiano inayoongozwa na Meneja wake Abdallah Msika aliyewahi kuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga imefanya marekebisho makubwa kwa wananchi
wanaozunguka mgodi huo hali iliyofanya kuimarisha usalama eneo la mgodi.
Alisema hivi sasa hata
watumishi wa ndani ya Mgodi wanaishi kwa amani huku vijijinii kwa wananchi
kwakuwa migogoro yote inayojitokeza idara ya mahusiano huifanyia kazi mara moja
kwa kufanya mazunguzo ya amani na wananchi.
Kwa upande wake Msika
alisema lengo la Idara yake ni kuleta mahusiano kwenye vijiji vinane
vinavyozunguka eneo la Mgodi huo bila kuwa na upendeleo wa kijiji Fulani
kwakuwa wote ni watoto wanaopaswa kupata huduma zinazofanana.
Msika alisema Mgodi wake
umejikita zaidi kusaidia huduma za kijamii katika sekta za Maji,kwa kuchimba
kisima kirefu cha pamp kila kijiji,kupanua zahanati na vituo vya afya pamoj na
kuboresha vyumba kwenye Shule za Msingi na Sekondari zinazozunguka eneo la
mgodi huo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI