BAADHI ya wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakiwa katika ofisi za Jimbo la Kahama,ambazo zimevun jwa na nyaraka muhimu zikitoweka huku zingine zikichanwachanwa. |
MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Kahama,Juma Ntahimpera akiongea na simu mbele ya ofisi za Jimbo za Chama hicho ambazo zimevunjwa na kuibiwa nyaraka huku zingine zikichanwachanwa. |
KATIBU wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Jimbo la Kahama;Michael Kigenda,akiwa katika ofisi za chama chake na kushuhudia uharibifu uliofanywa wa kuiba nyaraka muhimu huku zingine zikichanwa. |
KATIBU wa Baraza la Wazee wa CHADEMA jimbo la Kahama;Michael Kigenda,akikagua kutambua atahari iliyopatikana baada ya ofisi za Jimbo kuvunjwa. |
BANGO lenye anuani za ofisi za CHADEMA Jimbo la Kahama. |
BAADHI ya wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Ahmed Nambo wakitafakari jambomaeneo ya ofisi hizo. |
WAFUASI na Wanachama wa CHADEMA wakiwa mbele ya ofisi yao iliyovunjwa |
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakitoa samani za chama nje ya ofisi ya Jimbo |
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakitoa samani za chama nje ya ofisi ya Jimbo
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakipakia kwenye toroli samani za chama nje ya ofisi ya Jimbo tayari kwa kuzihamishia ofisi za wilaya.
NYARAKA zilizochanwa chanwa ndani ya ofisi za Jimbo la Kahama,anayebofya bofya simu ni RED BRIGED;Mandago.
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakishuhudia nyaraka zilizochanwa.
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakishuhudia uharibifu uliofanywa katika ofisi zao.
WAFUASI wa CHADEMA mjini Kahama wakishuhudia nyaraka zilizochanwa.
MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera akizungumza mbele ya ofisi za Jimbo.
MWENYEKITI wa CHADEMA wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mbele ya ofisi za Jimbo. |
WAFUASI na baadhi ya wanachama wakiwa katika butwaa baada ya uhalifu uliofanyika wa kuvunjwa na kuibiwa kwa nyaraka muhimu za CHADEMA |
WAFUASI
na baadhi ya wanachama wakiwa katika butwaa baada ya uhalifu
uliofanyika wa kuvunjwa na kuibiwa kwa nyaraka muhimu za CHADEMA |
WAFUASI
na baadhi ya wanachama wakiwa katika butwaa baada ya uhalifu
uliofanyika wa kuvunjwa na kuibiwa kwa nyaraka muhimu za CHADEMA |
RED BRIGEDI;Mandago |
RED BRIGERD;Mandago akiwa amebutwaa baada ya uhalifu
uliofanyika wa kuvunjwa na kuibiwa kwa nyaraka muhimu za CHADEMA |
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo
“CHADEMA”wilaya ya Kahama,kimemtimua uanachama Diwani wake sambamba na uongozi
wa jimbo huku nao wakikabidhi ofisi kwa staili ya aina yake ya kuchanachana
nyaraka za ofisi.
Mwenyekiti wa
CHADEMA wilaya ya Kahama;Juma Ntahimpera,alisema wamewavua uanachama kwa
kufuata taratibu,kanuni na sheria kwa mujibu wa Katiba ya chama ambapo awali
waliwapatia siku 14 za kujieleza kwanini wasifukuzwe uanachama kwa utovu wa
nidhamu na kutowajibika.
Ntahimpera alisema
uamuzi huo umefikiwa na Baraza la Mashauriano la wilaya lililokutana hivi
karibuni baada ya kuamua kuwajadiri viongozi hao kutokana na mwenendo wao ndani ya chama
kukiuka maadili,kanuni na katiba ya chama hicho.
Aliwataja
waliovuliwa uanachama na kukabidhiwa barua za Februari 13,mwaka huu kuwa ni
Diwani wa Kata ya Majengo;Bobson Wambura,ambaye pia alikuwa akishikilia wadhifa
wa Katibu Mwenezi wa Chama hicho Jimbo la Kahama.
Alisema Baraza pamoja
na mambo mengine lilijadiri mwenendo wa Diwani huyo ambaye mara nyingi amekuwa
akikashifu chama kuwa hakina mchango wowote na wadhifa alionao ambao ameupata
kutokana na umaarufu alionao katika jamii na si kwa nguvu ya chama.
Aliwataja
waliovuliwa uanachama sambamba na Diwani huyo kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya
kukihujumu chama ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo;Israel Barakiel,Katibu wa
Jimbo;Vicent Kwilukilwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Jimbo la Kahama
“BAWACHA”;Kasigwa Adram.
Wengine waliovuliwa
unachama ni Mratibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA “BAVICHA” wilaya ya
Kahama;Vicent Manyambo,na Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Kahama;Benedict Shija
ambapo walikabidhiwa barua zao Februari 13 mwaka huu huku ofisi zikifungwa na
kutakiwa kufika siku inayofuata kwa makabidhiano ya mali za chama.
Hata hivyo ilidaiwa
walikaidi maagizo ya kukabidhi mali
za chama na ofisi kwenye uongozi wa Baraza la Wazee wa Jimbo badala yake
kuzivunja ofisi hizo usiku na kutoweka na nyaraka muhimu huku zingine
wakizichanachana.
Katibu Baraza la
Wazee wa Jimbo la Kahama;Michael Kigenda alisema akiongozana na wajumbe wenzake
walishtushwa na hali waliyoikuta katika ofisi hizo walipofika saa nne kwa ajili
ya makabidhiano hivyo kulazimika kutoa taarifa kwa uongozi wa wilaya baada ya
kubaini ofisi zilikuwa zimevunjwa.
Ntahimpera alisema
baada ya kushuhudia uhalifu uliofanyika waliwapigia simu waliowafukuza ambao
hawakutaka kupokea simu hivyo kulazimika kutoa taarifa katika jeshi la polisi
kwa hatua zaidi za kisheria.
Katibu wa Baraza la
wazee wa Jimbo la Kahama alisema katika ukaguzi wa nyaraka zilizochanwa
hawakubahatika kuona masalia ya kitabu cha orodha ya wanachama na anuani zao jambo
ambalo wamelihusisha na majigambo wanayosadikiwa kuyafanya waliowafukuza kuhusika
kujiunga na chama kipya cha kisiasa kilicho katika mchakato wa usajili.
“Kuna madai kuitumia
ofisi kwa shughuli za chama hicho kipya huku wakijinadi watawabadili wanachama
wote wa jimbo la Kahama kwakuwa wana anuani zao ili kuhakikisha wanaiathiri
CHADEMA.”Alisema Kigenda.
Alipopigiwa simu
Diwani wa Kata ya Majengo;Bobsoni Wambura,hakutaka kutoa ushirikiano zaidi ya
kusema yupo mazingira mabaya na kwamba atapiga simu baadaye kutoa ufafanuzi
huku akidai kama ataondoka CHADEMA haitabaki
salama.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI