MABINTI wakishiriki katika nyimbo |
MABINTI wakionyesha sanaa ya maigizo |
WAKIONYESHA sanaa ya maigizo |
WAKISHIRIKI mchezo wa kandanda ili kujinusuru na ushawishi wa kujiingiza katika vitendo vya ngono.
UKOSEFU wa elimu ya kijinsia kwa wasichana kati ya umri wa miaka 10 na 19 wilayani Kahama ndio chanzo cha miongoni mwao zaidi ya 700 kuzaa katika umri mdogo.
Hayo yalibainishwa jana mjini Kahama na wasichana hamsini kutoka Kata za Mhongolo,Busoka,Shilela na Lunguya katika mafunzo ya elimu ya afya ambapo walisema idadi kubwa miongoni mwao hasa wanaoishi vijijini hawana elimu ya jinsia,na kuwa chanzo kwao kupata ujauzito katika umri mdogo.
Wasichana hao ambao wapo katika mpango wa kuwezeshwa ujasiriamali na Shirika la Kiota Women Healthy Development “KIWOHEDE” walisema ukosefu wa elimu hiyo huwafanya wajiingize kwenye mapenzi wakiwa na umri mdogo bila kujua madhara yake,ikiwemo kukatisha masomo yakiwemo ya sekondari na msingi.
Mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo;Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama;Kalidushi Charles alisema tatizo la Balehe kwa wasichana wasiokuwa na elimu ya jinsia ni hatari kwa umri mdogo.
Alisema hali ya kubadili umri kutoka utotoni na kuingia kwenye balehe kwa wasichana kuna hali ya kuhamasisha kufanya mapenzi hali ambayo kwa msichana ni mtihani ambao lazima aushinde vinginevyo ndio hujitokeza hali ya mimba zisizokuwa za lazima.
Kufuatia hali hiyo Charles aliwataka ili kuzuia hali hiyo ni
kujibidisha na njia za kuzuia hali hiyo ikiwemo shule na michezo ambayo husukuma umri wa kuanza kufanya mapenzi unakuwa mkubwa kwakuwa muda mwingi utautumika kwenye mambo hayo ya kielimu na michezo.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE;Justa Mwaituka alisema tatizo la uzazi chini ya umri mdogo wilayani Kahama ni kubwa kwakuwa katika Kata nne tu kati ya 53 zilizopo wilayani Kahama wamepatikana wasichana zaidi ya Elfu moja waliozaa chini ya umri mdogo.
Mwaituka alisema idadi hiyo inapatikana kutoka ngazi ya Kata tu pasipo kuingia kwenye mashina hali ambayo idadi ingeweza kuongezeka zaidi iwapo kama wangejikita hadi katika ngazi hizo za chini na kuongeza inatakiwa jitihada za ziada ili kupunguza tatizo hilo wilayani Kahama.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI