BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
|
WASHIRIKI waliohudhuria semina juu ya kujitambua katika kupambana na maambukizi mapya ya UKIMWI na kupatiwa elimu stahiki ya maradhi hayo,ambayo iliandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la HUHESO FOUNDATION yenye makao makuu yake Kata ya Malunga katika Halmashauri ya Mji Kahama,wakiimba wimbo wa hamasa |
|
WASHIRIKI wakijadili. |
|
WAHIRIKI wakisikiliza kwa makini |
|
MSHIRIKI akichangia hoja. |
|
MWEZESHAJI katika semina hiyo,Afisa Muuguzi Mkuu katika Halmashauri ya Mji Kahama;Richard Mabagara Kajogo,akitoa mada juu ya Ushauri Nasaha. |
|
WANAUME ambao ni washiriki katika semina hiyo. |
|
ATHUMANI Ally kulia akiwa na Mwenzake wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mwezeshaji kuhusiana na Elimu ya UKIMWI |
|
MIONGONI mwa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa CARITAS mjini Kahama. |
|
BAADHI ya Washiriki katika Semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la HUHESO FOUNDATION la wilaya ya Kahama |
|
MSHIRIKI katika semina hiyo;Samson Aloyce akiandika maelezo juu ya Elimu ya UKIMWI na kujitambua kwa mwanaume katika kupambana na maambukizi mapya ya maradhi hayo. |
IMEELEZWA kuwa wanaume wengi hawapendi kupima
UKIMWI sambamba na kuogopa kuambatana na wake zao hospitalini kwa lengo
kutazama afya zao zaidi ya kuwatumia kama
chambo kipindi cha ujauzito kujitathimini
iwapo wameathirika.
Hayo
yalibainishwa na mkufunzi mkuu kitengo cha UKIMWI kutoka katika
hospitali ya Halmashauri ya mji Kahama bi. Emerenciana
Machibya katika semina ya siku mbili ya kutambua ufahamu
kuhusu VVU na UKIMWI kwa wanaume wanaofanya kazi migodini pamoja na madreva wa
magari makubwa.
Katika semina hiyo iliyoandaliwa na shirika la
HUHESO FOUNDATION la wilayani Kahama chini ya ufadhili wa Rapid Fund Envelope “RFE”
ya jijini Dar Es Salaam iliyolenga kuwapatia elimu ya UKIMWI wanaume
hao,Mkufunzi huyo alisema wanaume hufanya kosa kubwa kujitathimini ni wazima
ama wameathirika kupitia vipimo walivyofanyiwa wake zao.
“Napenda mtambue unaweza kuathirika mwenza wako akawa
hajaathirika,ama mpenzio akaathirika ukawa mzima cha msingi ili kubaini uhakika
ni wote kujitokeza kupima.”Alisema bi Machibya.
Aidha bi.
Machibya alisema kuwa tafiti inaonyesha kuwa wanaume wengi
hapa nchini hawapendi kupima vvu mara kwa mara ili kujua afya zao, na kuwasii
wakinababa waache maramoja tabia ya kuwatanguliza wakina mama
hospitalini kupima vvu, na badala yake wawe mstari wa mbele kuambatana na wake
zao kwenda kuangalia afya zao.
Alisema faida
ya kupima mara kwa mara husaidia kipindi wanapogundulika kuwa na maambukizi
mapya ya virusi vya UKIMWI kuweza kupata ushauri nasaha na kumudu kuanza kutumia mapema dawa za kufubaza virusi .
Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi
wa HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa alisema ili kukabiliana na janga hilo ni
vema wanaume kuwa na mpenzi mmoja aliye mwaminifu , kutumia kondomu wakati wa
kujamiiana au kuacha kabisa.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI