Thursday, January 16, 2014

MUME AMWAGIA TINDIKALI MKE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MARIA Nkwabi [33]akiwa katika wodi ya Majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambapo anapatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa tindikali na Mumewe.

MARIA Nkwabi akipatiwa alipokuwa akisubiria usafiri wa kumfikisha hospitali ya wilaya ya Kahama kupatiwa matibabu mara baada ya kumwagiwa tindikali na mumewe katika ugomvi wa kugombea mali.
MKAZI mmoja wa Kijiji cha Kakola wilayani Kahama;Maria  Nkwabi [33] amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kumwagiwa Tindikali na Mumewe;Ray Chobe katika ugomvi unaodaiwa kugombea mali.

Akiongea katika wodi ya majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Kahama;mwanamke huyo alidai kuwa wamekuwa katika ugomvi wa mara kwa mara juu ya matumizi ya fedha baina yake na mumewe ambaye pamoja na mafanikio ya kimaisha waliyokuwa wameyapata alianza tabia ya kufuja mali hadi kuufikia kufirisika.

Alisema baada ya mumewe kufuja mali alianza tabia ya kulazimisha kuchukua fedha za mgahawa anaoumiliki kitende ambacho alikivumilia kwa muda mrefu na siku ya tukio alipogoma kumpatia fedha aliondoka na aliporejea alilazimisha apewe pesa alipogoma ndipo alipomwagia Tindikali.

Alifafanua baada ya kumwagiwa tindikali hima alikimbilia kwenye ndoo ya maji na kukiinamisha kichwa chake ndani ya maji ili kujinusuru asidhurike zaidi ya kemikali hiyo huku akimuacha mumewe akichukua fedha za mauzo na kutokomea kusikojulikana.

Polisi wilayani Kahama wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na jitihada za kumpata mwanaume aliyehusika na unyama huo bado unaendelea.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI