Saturday, December 28, 2013

TAMAA YA MAPENZI HUSABABISHA NGONO ISIYO SALAMA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MKURUGENZI wa The Foundation for Human Healthy Society "HUHESO FOUNDATION";Juma Mwesigwa,akiongea jambo katika Semina inayowahusisha wanaume wafanyao kazi migodini na madreva wa magari makubwa,juu ya kujitambua na elimu ya UKIMWI.
MWEZESHAJI katika semina hiyo;Afisa muuguzi katika hospitali ya wilaya ya Kahama;Emerenciana Michael Machibya akitoa somo juu ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa jamii,pembeni yake ni Mwezeshaji mwenzake;Afisa Muuguzi Mkuu Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagara Kajogo.
 MSHIRIKI katika semina hiyo;Rajabu Peter "Rachi"akishiriki kikamilifu katika semina hiyo kwa kuchangia hoja.

MWEZESHAJI katika semina hiyo;Afisa Muuguzi Hospitali ya wilaya ya Kahma;Emerenciana Michael Machibya,akitoa somo la ufahamu zaidi juu ya Elimu ya UKIMWI,hususani juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI.

 I - Dan Mwahengera mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia hoja.

MMOJA wa  Wawezeshaji katika semina hiyo;Afisa Muuguzi Mkuu katika Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagara Kajogo akiwasilisha mada.
WASHIRIKI wa semina hiyo iliyowahusisha wanaume ambao ni madreva wa magari makubwa na watumishi wa migodini.

MIONGONI mwa washiriki katika semina iliyowahusisha wanaume ambao ni madreva wa magari makubwa na watumishi wa migodini;Haruna Bakari naye akishiriki ipasavyo katika semina hiyo kwa kuchangia hoja.

 AFISA Muuguzi katika hospitali ya wilaya ya Kahama;Emerenciana Michael Machibya,ambaye ni mwezeshaji katika semina hiyo akifafanua jambo.

STEPHEN Mhola naye akichangia hoja.

AFISA Muuguzi katika Hospitali ya wilaya ya Kahama;Emerenciana Michael Machibya,akiwafafanulia kwa msisitizo washiriki katika semina hiyo juu ya masuala mbalimbali ya Elimu juu ya UKIMWI.

RACHI akichangia hoja kwa umakini.


TATIZO la matumizi sahihi ya Kondomu limedaiwa kusababishwa na tamaa ya wanaume ambao idadi yao kubwa hushindwa kujizuia kutembea kimapenzi na wanawake pindi wanandoa wao wanapokuwa hawapo.

Hayo yameelezwa leo mjini Kahama na Mwezeshaji wa mafunzo juu ya kujitambua na elimu ya ukimwi kwa wanaume,bi Emarisiana Machibya,ambapo amedai wanawake wanao uwezo wa kuvumilia kutofanya mapenzi kwa muda mrefu tofauti na wanaume.

Mafunzo hayo yameandaliwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya The Foundation for Human Health Society ( HUHESO FOUNDATION) ya wilayani Kahama na kuwashirikisha wanaume 60 kutoka migodini na madreva wa magari makubwa.

Katika mafunzo hayo imeelezwa wanaume wengi wana matamanio wanapoona wanawake hali inayowafanya wakose muda wa maandalizi ya matumizi ya kondomu na kupelekea kufanya ngono zisizo salama.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa asasi ya HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa,mafunzo hayo ni muendelezo wa mradi wao wa kuwaokoa wanawake na wasichana wanaofanya biashara ya ngono na kuishi katika mazingira magumu dhidi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa UKIMWI.

Mwesigwa amesema katika mradi huo pia wanawake hao watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali itawafanya wawe na miradi ya kujikwamua kiuchumi na kuondokana na biashara hiyo ya ngono ambayo ni hatari katika maisha yao.


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI