VIJANA wa stendi kubwa ambao ni wapiga debe wakipumzika baada ya awamu ya kwanza kushindwa kuitoa gari hiyo iliyokuwa imezama.
WAPIGA debe wakianza jitihada za kuitoa gari hiyo iliyokuwa imezama
VIJANA wakiendelea na kupambana ili kuinasua gari hyo iliyokuwa imezama .
BAADHI ya watu wakishuhudia wakati vijana kutoka stendi kubwa walipokuwa wakipambana kuitoa gari iliyokuwa imezama.
VIJANA hao almaarufu kama wapiga debe wakimfukuza mwenzao Baunsa baada ya kutaka kuwadhurumu haki yao.
BAUNSA chini ya ulinzi wa wenziwe waliomtaka atoe fedha kwa hiari kabla hawajaanza kumshushia kipigo
KICHAPO kilianza kama rasharasha ya mvua baada ya Baunsa kugoma kutoa Shilingi Elfu Tano.
WASAMARIA wema wakiingilia ugomvi wa vijana wapiga debe waliogeuza uwanja huo ni wa vita baada ya kutaka kudhurumiana.
MVUA kubwa ambayo
imenyesha mwishoni mwa wiki mjini Kahama imesababisha kizaa zaa baada ya
kuharibu miundo mbinu ya barabara kiasi cha gari kuzama huku kijana mmoja
akitaka kupokonywa uhai wake na wenzake sababu ya Shilingi Elfu tano baada ya
kuikwamua gari iliyokuwa imezama.
Tukio hilo la aina yake
lilitokea Desemba 14;mwaka huu,katika viunga vya uwanja wa Barcelona mkabala na
Ofisi za Kampuni ya usafirishaji abiria;Mohammed Trans,baada ya gari aina ya
Mark Two yenye namba za Usajili T 532 BHJ kuzama katika mashimo makubwa
yaliyotokana na mvua hiyo,iliyonyesha
kwa takribani saa moja mnamo saa tisa alaasiri.
Baada ya gari hiyo kuzama
kwa kuzidiwa na wingi wa maji yaliyokuwa tatizo kwa upitikaji wa magari
mbalimbali kutokana na kuonekana kama ni mto,dreva wa gari hiyo Mika Moshi
aliamua kwenda kuomba msaada kwa vijana wahusikao na kupiga debe katika kituo
kikuu cha abiria wilayani Kahama,ambao walifika na kutumia takribani dakika 15,kuiondoa
toka katika lindi la maji hayo.
Dreva wa gari hiyo alitoa shukrani
ya kutolewa gari kwa kuwapatia Shilingi Elfu Kumi,ndipo kilipoibuka kizazaa
baada ya kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Baunsa kuwapatia wenzake Shilingi Elfu tano ili
wagawane nae kukimbia na kiasi kama hicho jambo ambalo wenzake hawakuliafiki na
kumfukuza na mara walipompata walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
Hata hivyo Baunsa alinusuriwa kutolewa uhai na wenzake na
baadhi ya watu waliotumia hekima kuwaaamua kisha kuwasihi fedha hiyo wagawane
pasipo kupunjwa miongoni mwao jambo ambalo walilitekeleza.
Chanzo cha habari ni Jackson
William.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI