Saturday, December 14, 2013

HUHESO YAFUNDISHA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

WASHIRIKI katika semina yenye lengo la kuwaelimisha Wasichana na Wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wanaoishi katika mazingira magumu iliyofanyika katika Ukumbi wa Caritas mjini Kahama,iliyoandaliwa na shirika la HUHESO FOUNDATION chini ya ufadhili wa RFE ya jijini Dar Es Salaam wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa semina hiyo;Tabibu Kaskile Jumanne.

BAADHI ya washiriki 60 waliohudhuria semina hiyo wakibadrishana mawazo.

 MKURUGENZI wa Shirika la HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa akiongea na washiriki 60 wa semina iliyokuwa na lengo la kuwapatia elimu juu ya kukabiliana na maambukizi mapya ya Ukimwi na matumizi sahihi ya mipira ya kiume na kike.

 MWEZESHAJI katika semina hiyo;Tabibu Kaskile Jumanne akiwaelekeza washiriki juu ya matumizi sahihi ya kondomu ya kiume.

 MMOJA wa washiriki katika Semina hiyo;Coletha akichangia hoja.

MWEZESHAJI katika semina hiyo tabibu Kaskile Jumanne akitoa ufafanunuzi juu ya matumizi ya kondomu ya kike,aliyoishika katika mkono wake wa kushoto.

 MWEZESHAJI katika semina hiyo;Kaskile Jumanne ambaye ni tabibu kutka hospitali ya wilaya ya Kahama na Mkufunzi wa wawezeshiji wa Ushauri Nasaha akielekeza matumizi sahihi ya uvaaji wa Kondomu ya kiume.

WASHIRIKI katika semina hiyo wakikumbushana juu ya hatua ya kwanza ya matayarisho ya kuvaa kondomu ya kike.

MSHIRIKI katika semina hiyo;Joyce akifungua kondomu ya kike.

MWEZESHAJI Tabibu Kaskile Jumanne akiwaonyesha washiriki wa semina kondomu.

MSHIRIKI Stella akimakabidhi mshiriki mwenzie kondomu ya kiume.

 MRATIBU wa shirika la HUHESO FOUNDATION;Jackline Kamayugi akimuonyesha mwandishi wa habari wa gazeti la Mzawa;Paul Kayanda kondomu ya kike,anayeshuhudia mwenye shati la bluu ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION;Gabriel John.


IMEELEZWA kuwa wanawake kutokuwa na maamuzi juu ya tendo la ndoa sambamba na matumizi mabaya ya kondomu za kike na kiume ni sababu ya kuwepo kwa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi katika jamii.

Hayo yalielezwa na Mwezeshaji katika semina juu ya mapambano ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi yaliyowahusisha wasichana na wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wanaoishi mazingira mangumu,Tabibu Kaskile Jumanne;ambapo alisema wanawake wengi ni waathirika kutokana na woga wao wa kumiliki ngono.

Tabibu Jumanne alisema wanawake hujikuta katika maambukizi mapya kutokana na kutokuwa majasiri wakati wa tendo la ndoa kwa kushindwa kumuongoza mwanamume katika masuala ya kuvaa kondomu na maamuzi hayo kumuachia mume ambaye ndio huwa mwenye maamuzi wa kutumia ama kutotumia.

Alisema kutokana na maamuzi ya utekelezaji ngono kuwa kwa mwanamume huku mwanamke akishiriki kama mtumwa wa mapenzi kutokana na aibu ambao ni utamaduni asilia wa Mtanzania hujikuta akiambukizwa Virusi vya Ukimwi pindi mwenzi aliyenaye akiamua kutenda tendo hilo pasipo kondomu.

Aliendelea kusema kuwa hata kama akikutana na mwanaume mwenye dhamira ya kutumia kondomu hujikuta katika hatari ya kupata maambukizi kutokana na mwanaume kutotambua matumizi sahihi ya kondomu ama kutokana na kuwa amelewa ama kutotambua kabisa juu ya uvaaji na uvuaji sahihi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa ambaye shirikala lake ndio lililoendesha semina hiyo kwa ufadhili wa RFE,alisema wanawake wanapaswa kubadilika na kuondokana na jukumu la mapenzi kutawaliwa na mwanaume ili kuondokana na hatari ya kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Mwesigwa alisema shirika lake hivi sasa linatekeleza mradi wa kuwakomboa akina dada wanaohusika na biashara ya ngono na wanaoishi katika mazingira magumu,ambapo huwapatia elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya cherehani na katika semina hiyo imewashirikisha washiriki 60 kutoka makundi hayo ambao wamewapata kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI