Wednesday, December 25, 2013

AFUNGWA MIAKA 24 KWA WIZI, KUKUTWA NA SARE ZA POLISI NA SILAHA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




 MAHAKAMA ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu kwenda jela
miaka 24 mkazi wa Bariadi;Luteja Magembe  baada ya kupatikana na hatia
ya makosa matatu likiwemo la kukutwa na sare za askari Polisi sambamba
na silaha zihusikazo na kufanyia uhalifu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo;Oguda Robert, ameridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka na
kutoridhishwa na ule wa mtuhumiwa hivyo kumtia hatiani,ambapo kwa
Kosa la kwanza la kukutwa na sare za polisi kinyume cha sheria atawajibika kutumikia kifungo cha miaka mitatu chini ya kifungu no,257 kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.

Hakimu Robert alisema mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka saba jela chini ya kifungu namba 265 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kutokana na kosa la pili la kuvunja na kuiba,huku Kosa la tatu la kupatikana na silaha mbali mbali za
kubomolea nyumba nalo amehukumiwa miaka 14 chini yakifungu no,268
kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002. 
Hakimu Oguda alisema baada ya Mahakama kumtia hatiani mtuhumiwa inatoa hukumu hiyo  ili iwe fundisho kwa
watu wenye tabia kama hizo.

Mshtakiwa kabla ya kusomewa hukumu hiyo alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba kusamehewa kwakuwa alitenda kosa hilo pasipo kutarajia na kwamba hakutaka kuipa usumbufu Mahakama kusikiliza shauri lake kwa kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni la kwanza kutenda katika maisha yake.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu na hakimu aliyesikiliza kesi hiyo;Robert
Oguda,mtuhumiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba mahakama
imuonee huruma kwa kuwa kuna watu wanaomtegemea.

Baada ya maombi hayo Mwendesha Mashtaka katika kesi hiyo,Mkaguzi wa Polisi Samweli Kirabuka alipinga vikali maombi hayo na kuiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa   alitenda makosa mawili ya kuvunja na
kuiba huku akitumia sare za Jeshi la Polisi jambo ambalo ni kinyume
cha sheria na anastahili kupatiwa adhabu kali ambayo itakuwa funzo kwa
watu wengine wenye tabia ama wenye dhamira ya kufanya uhalifu.

CHANZO CHA HABARI HII  NI GABRIEL MUHINDI.


 


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI