MAHAKAMA ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu kwenda jela miaka
saba mkazi mmoja Luhaga Saida Mwangile [20]baada ya kumtia hatiani kwa kosa wizi wa pikipiki.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI
Hukumu hiyo ilitolewa na
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo;Oguda Robert,baada ya kusikiliza pande zote mbili
za mlalamikaji na mshitakiwa ambaye alikiri kutenda kosa la wizi wa pikipiki
aina ya King Lion yenye usajili namba T 696 CJF mali ya Meshaki Henry mkazi wa
mjini Bariadi.
Mstakiwa alidaiwa kutenda
kosa hilo Novemba 15, mwaka huu kisha kutoweka nayo lakini jitihada za Jeshi la
Polisi zilifaulu kumkamata Mwangile Novemba 19,mwaka huu katika kijiji cha
Nyasululi,wilaya ya Bunda mkoani Mara na kusomewa shuari lake kwa mara ya
kwanza katika mahakama hiyo Novemba 20.
Akisoma hukumu hiyo,Hakimu
Robert alisema baada ya Mahakama kujiridhisha mshtakiwa kuwa anakosa,inamtia
hatiani na kutoa adhabu inayolingana na kosa lake ili liwe funzo kwake na kwa
jamii ambayo imekuwa ina dhamira ya kufanya uhalifu na unaolingana na huo.
Mshtakiwa kabla ya
kusomewa hukumu hiyo alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba kusamehewa
kwakuwa alitenda kosa hilo pasipo kutarajia na kwamba hakutaka kuipa usumbufu
Mahakama kusikiliza shauri lake kwa kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni la
kwanza kutenda katika maisha yake.
Baada ya maombi hayo
Mwendesha Mashtaka katika kesi hiyo,Mkaguzi wa Polisi Samweli Kirabuka alipinga
vikali maombi hayo na kuiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.