Friday, November 8, 2013

WASICHANA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WAFANYA MTIHANI WA UFUNDI CHEREHANI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MWALIMU wa Ufundi wa kushona nguo ama Ufundi cherehani,Madamu Stella akisimamia mtihani

BAADHI ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu waliokuwa wakijifunza ufundi wa kushona nguo wakifanya mtihani

 ALIYESIMAMA na bahasha mkononi ni Madamu Stella akisimamia mtihani wa nadharia ya ufundi Cherehani kwa Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu.

 BAADHI ya wasichana hao wakifanya mtihani


 BAADHI ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu waliopatiwa mafunzo ya Ujasiriamali na ufundi cherehani na HUHESO FOUNDATION wakiwa katika chumaba cha mtihani



WASICHANA 24 wanaoishi katika mazingira makubwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama,ambao kwa kipindi cha miezi mitatu wamepatiwa mafunzo ya Ujasiriamali na Ufundi Nguo “Ufundi Cherehani” na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation For Human Health Society “HUHESO FOUNDATION” wafanya mitihani ya kuhitimu mafunzo yao.

Wasichana hao walifanya mtihani wa nadharia wa ufundi cherehani katika darasa linalomilikiwa na HUHESO FOUNDATION yenye makao makuu yake Kata ya Malunga katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,ambapo wasichana hao watahitimu mafunzo yao Novemba 16,mwaka huu baada ya kukamilisha kozi yao iliyo chini ya Mradi wa HUHESO FOUNDATION uitwao;An Action on young girls sexual exploitation project,unaofadhiliwa na Shirika la Rapid Funding Envelope “RFE” ya jijini Dar Es Salaam.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI