Duuh Wasanii wa Segere mchezo huu ni maadili ya Kitanzania?
JAMII nchini imeaswa kuzingatia mila, desturi na utamaduni wa
makabila ya hapa nchini kuliko kuenzi
utandawazi ambao unaathiri nidhamu na uzalendo wa Mtanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani
Kahama ; Ezekieli Maige ,katika uwanja wa Halmashauri ya mji wa Kahama
alipoongea na watu wa rika mbalimbali,wakati wa uzinduzi wa michuano ya ngoma
za asili.
Akiwasilisha ujumbe huo kwa niaba ya Mbunge huyo ,Diwani wa
kata ya Lunguya ;Benedict Manuali
amesema , kizazi cha sasa kimeathiriwa
na utandawazi kiasi cha kutishia kuendelea kuwepo kwa uzalendo wa Taifa.
Amesema Taifa
linakabiliwa ombwe la upotofu wa vijana wengi kukosa nidhamu kwa jamii kunakochangiwa
kwa kiwango kikubwa na Utandawazi huku jamii inayostahili kuongoza,kusahau
misingi ya malezi inayoambatana na kuzingatia mila na desturi za makabila ya Kitanzania.
Ameowamba Watanzania bora wakabadilishana uzoefu wa mila na
desturi za kabila moja hadi lingine ili kudumisha nidhamu,maadili na uzalendo
wa nchi kuliko kuiga masuala yatokanayo na utandawazi ambayo yanaathiri utaifa
wetu.
Amekumbusha kuwa utandawazi si mbaya pindi ukitumika kwa
masuala ya msingi ya kusukuma maendeleo ya Taifa na si kuiga tamaduni za
ughaibuniambazo ni chanzo cha kuathiri uzalendo wa Watanzania.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI