Mwenyekiti wa taifa wa taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation;Khamis Mgeja,akiongoza kuzindua Filamu ya Msanii Madebe Jinasa kwa kununua CD kwa Shilingi Laki Tano Taslimu ili kuchangia maendeleo ya Msanii huyo katika kuendeleza Mila,Desturi na Utamaduni wa Mtanzania.
JAMII imetakiwa kuendeleza mila,utamaduni na desturi
za Mtanzania ili kuliepusha Taifa
kuyumba na kutishia kutoweka kwa uzalendo hali itakayosababisha machafuko yatakayotokana na mmomonyoko wa
maadili unaochangiwa na kuendekeza utandawazi.
Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi
ya Tanzania Mzalendo Foundation;Khamis Mgeja,wakati akizindua Filamu ya Msanii
maarufu wa nyimbo za asli kanda ya Ziwa na Magharibi;Madebe Jinasa katika
uwanja wa Shule ya Msingi Nhele kata ya Lusu wilayani Nzega.
Mgeja alisema hivi sasa nchi ipo katika ombwe la
kuyumba kimaadili kunakotokana na kuanza kupotea kwa mila,desturi na utamaduni
kutokana na kugubikwa na utandawazi unaopandikiza mila na desturi za kutoka
ughaibuni.
“ Tukiziacha mila na desturi taifa letu litayumba sana ,wenzetu kama nchi ya China wamepiga hatua za maendeleo
kwa kudumisha mila na desturi kwa hiyo hizi mila lazima tuzienzi,"Alisema
Mgeja.
Aidha aliomba Serikali kupitia TAMISEMI kuandaa
mkakati mkubwa kupitia Halmashauri kuwawezesha malenga nchini kudumisha mila na
desturi kupitia sanaa zao ili jamii ione umuhimu wa kudumisha na kuendeleza
mila na desturi.
Habari na Ali Lityawi na Zengo Saida.