IMEELEZWA kuwa Ajali 29 za
Barabarani kati ya 45 mkoani Simiyu zimesababisha vifo 33 kati ya mwezi January hadi Agosti mwaka huu,huku
16 zikisababisha majeruhi 28 waliolazwa katika hospitali za wilaya za
Bariadi,Meatu,Itilima,Busega na Maswa.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoani Simiyu katika ufunguzi wa
wiki ya nenda kwa usalama ambapo kitaifa inafanyika Mkoa wa Mwanza kuanzia
tarehe 23/09/2013.Ilibainisha Vyanzo
vya ajali Barabarani vinatokana na ulevi,mwendo kasi kwa madreva wa magari
na pikipiki sambamba na kuwepo kwa
miundo mbinu mbovu ya barabara inayosababishwa na hali ya hewa ( mvua ).
Aidha ilibainishwa chanzo
kingine ni kukosekana kwa alama za
usalama barabara kwa baadhi ya maeneo kiasi ambacho madereva kutoelewa
maangalizo ya barabara kama vile kukiwa na
kona kali, daraja ,mlima na mteremko.
Taarifa hiyo iliwataja baadhi
ya waendesha pikipiki kuwa chanzo cha ajali ambazo zingeliweza kuzuilika
kutokana na tabia yao
ya kuwakimbia askari wanaokuwa doria kwa kutumia pikipiki ama magari ya polisi hukimbia
kwa mwendo mkali na kujikuta wakisababisha ajali.
Ilibainisha zaidi kuwa chanzo
cha vitendo hivyo nikukosekana kwa elimu
ya usalama barabarani miongoni mwa wahusikao na kuendesha pikipiki hizo na
hivyo Kitengo cha Polisi mkoa wa Simiyu kuanzisha mkakati wa kukabiliana na
hali hiyo,kwa kuanza kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kuanzia shule za msingi
,sekondari hadi waendesha vyombo vya moto,hali ambayo itasaidia kupunguza
ajali.
Hata hivyo taarifa hiyo iliziomba Halmashauri zote pamoja na
wanaohusika katika mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanaweka alama za barabarani ili
kupunguza ajali katika mkoa huo.
CHANZO CHA HABARI NI GABRIEL MUHINDI
BARIADI.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI