Sunday, September 15, 2013

WASICHANA WATAKA KUJITEGEMEA KWANZA NDIPO WAOLEWE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MKURUGENZI wa Kiota Women Health and Development Organisation "KIWOHEDE"ya Jijini Dar Es Salaam;Justa Mwaituka,akiwasikiliza kwa makini mabinti kutoka Kata ya Shilela,ambao walimthibitishia kuwa hawako tayari kuingia katika maisha ya ndoa hadi hapo watakapojijenga kimaisha.
WASICHANA wa Kata ya Shilela wenye umri wa miaka kumi hadi Kumi na Tisa,wakisikisliza kwa makini maelezo juu ya Mradi wa Kuwawezesha Wasichana walio Nje ya Shule,kutokana na kupata mimba ama kukosa mahitaji muhimu,kumudu kuwarejesha katika masomo ama kuwawezesha kupata stadi za maisha ili kumudu kushiriki shuguli za kiuchumi na kuwaingizia pato halali. 
Bi Justa Mwaituka Mkurugenzi wa KIWOHEDE akiwa amembeba binti Helena Paulo miezi tisa mtoto wa pili kwa Pili Shabani{ 18 }mkazi wa Shilela,moja ya majukumu ya Shirika la KIWOHEDE katika kutekeleza Mradi wake wa majaribio wa miaka mitatu katika Kata nne za wilaya ya Kahama ni kuwawezesha Wasichana wenye umri wa miaka Kumi hadi Kumi na Tisa kupata taarifa mbalimbali za huduma za Afya ya Uzazi ikiwemo Uzazi wa Mpango.
MKURUGENZI wa KIWOHEDE;Justa Mwaituka akiwa na wasichana wa Kata ya Shilela ambao hawako tayari kuolewa hadi hapo watakapojimudu kiuchumi.
MKURUGENZI wa KIWOHEDE Justa Mwaituka akiwa na baadhi ya wasichana ambao hawako tayari kuolewa hadi hapo watakapojijenga kiuchumi miongoni mwao wamo wasichana ambao wamepata ujauzito katika umri mdogo.

BAADHI ya viongozi wa kata na Wazee mashuhuri katika Kata ya Shilela waliohudhuria ufunguzi wa Mradi wa Kuwawezesha Wasichana walio nje ya shule.
FASTINA Kiluvia wa UNFPA ambao ni wafadhili wa KIWOHEDE akitoa mada.
Bi Rehema Kantabula kutoka wilaya ya Kahama naye akitoa mada
Emmanuel Yohana akiongoza kikao hicho

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI