Baadhi ya wanafunzi wa Rocken Hill Academy wakifutilia kwa furaha mahafari ya wenzao waliohitimu darasa la saba 2013
Wanakikundi cha taarabu katika Rocken Hill Academy wakiserebuka na wimbo murua wa mipasho wa kuwaaga vijana wenzao waliohitimu darasa la saba 2013.
Rocken Hill Academy ni nyumba ya vipaji hapa ni wasanii wa kundi la maagizo katika shule hiyo likionyesha igizo lililoteka hisia za waliohudhuria mahafari hiyo.
CHANGAMOTO kubwa inayoikabili jamii ya Watanzania ili kufikia Mafanikio kimaisha ni kukubali siku zote kuishi katika maisha ya kusaka elimu na maarifa mbalimbali.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Taasisi za Rocken Hill Academy na Anderlek Ridges Secondary School;Alexander Kazimil, katika mahafari ya kumaliza shule ya msingi kwa vijana wa Rocken Hill Academy iliyo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Alisema jamii ya Watanzania hususani vijana waliohitimu elimu ya msingi ni budi wakubali na wawe tayari kusaka maarifa mapya ndipo ndoto walizo nazo katika maisha zitafanikiwa.
Mkurugenzi huyo alisema na kusudi hayo wayafikie ni budi kuwe na msukumo kutoka kwa wazazi huku vijana nao wakizingatia misingi ya maadili ya asili pasipo kuhadaika na utandawazi ambao ukitumika visivyo utakuwa chanzo cha kuharibika kwa maisha ya vijana.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafari hayo Mkuu wa Polisi Mstaafu wa wilaya ya Kahama;George Simba,aliwataka vijana kutokubali kutumika kinyume na maadili ya Kitanzania kwa kukubali kutumiwa kama makontena ya kusafirisha madawa ya kulevya kwa tamaa ya utajiri wa haraka.
Aliwaasa vijana kuwafichua Wafanyabiashara watakaojitokeza na kuwashawishi kusafirisha madawa ya kulevya ama kutumia kutokana na biashara hiyo kutokukubalika katika jamii na ni chanzo cha kuvuruga hali ya amani iliyopo nchini.
Chanzo cha Habari;Hassan Lityawi na Rajab Peter. KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI