DIWANI WA KATA YA BUKANDWE LUTENI MSTAAFU HENLY MALISHI AKIONGEA NA WANANCHI WAKE. |
MENEJA WA KAMPUNI YA RESOLUTE AKIMKABIDHI MADAWATI DIWANI WA BUKANDWE. |
MWENYEKITI WA SHULE AKIMKABIDHI MADAWATI MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KANEGELE. |
WANANCHI WAKISHUHUDIA MAKABIDHIANO YA MADAWATI HAYO. |
Shule ya Msingi Kanegere
iliyopo kata ya Bukandwe Wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita imekabidhiwa madawati
31 kati ya 45 yaliyokuwa yatolewe ili kusaidia tatizo la upungufu wa madawati
mashuleni.
Makabidhiano hayo yamefanyika
leo katika shule ya msingi Kanegele ambapo Kampuni ya utafiti ya Resolute
imekabidhi madawati kwa Diwani wa Kata hiyo Luteni Henly Malishi ikiwa ni mradi
mmoja wapo ulikabidhiwa katika shule hiyo.
Meneja wa kampuni hiyo
William Harmworth amesema madawati yaliyokabidhiwa leo ni kati ya miradi minne
iliyopangwa kufanywa na kampuni kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambayo imeghalimu Milioni 47.7 .
Harmworth ameitaja miradi
mingine kama kisima cha pampu ya mkono karibu na shule,kukarabati chumba kimoja
cha darasa,kuezeka na kumalizia vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya Mwalimu
katika shule ya msingi Kanegele.
Amesema kuwa kampuni inapofanya
jitihada za kusaidia na jamii ni vizuri kuwepo na hali ya jamii pia
kushirikiana kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika eneo hilo.
Aidha Diwani wa kata hiyo
amewashukuru Resolute kwa mchango wao na kumtaka Mwalimu Mkuu kulinda na
kusimamia madawati hayo ambayo wamepunguza idadi ya upungufu wa madawati
yaliyokuwa yakihitajika shuleni hapo.
Michango mingine ambayo Resolute imechangia ni ununuzi
wa ekari 80 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari,ujenzi wa visima viwili cha
sekondali na kwa ajili ya kijiji kilichoko mita 60 kaskazini Magharibi mwa
shule ya msingi Kanegele.
Habari na Herieth Katikiro KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI