WASICHANA KUWEZESHWA KAHAMA
Shirika la Umoja wa
Mataifa la UNFPA litawasaidia zaidi ya watoto wa kike
300 walio katishwa masomo katika umri mdogo kati
ya miaka 10 hadi 19 na wamekuwa wakiishi kwenye
mazingira magumu wilayani Kahama , mkoani Shinyanga.
Ofisa kutoka
Shirika la UNFP ,Fatina Kiluvia alisema juzi wakati akitambulisha mradi
huo wilayani Kahama ambapo watoto wa kike watakao wezeshwa ni wale
waliokatishwa masomo na kuolewa katika umri mdogo ambao wamekuwa
wakiishi katika mazingira hatarishi.
Kiluvia alisema kufaatia
utafiti uliofanywa na Shirika hilo katika wilaya ya Kahama na Kishapu
mkoani Shinyanga ilibainika tatizo la watoto wa kike kukatishwa maosomo
na kuolewa katika umri mdogo limekuwa tatizo linalopelekea waishi katika
mazingira magumu.
Alisema mradi huo wa
kuwawezesha watoto hao wa kike ikiwemo kuwapatia elimu ya afya ya
uzazi , ujasiriamali utaanza kutekelezwa katika vijiji 19
kwenye kata nne za Shilela , Lunguya , Busoka , Mhongolo
wilayani Kahama na utashughulikiwa na Asasi ya kiraia ya Kiota
Women Health and Development Organization ( KIWOHEDE )
kwa ufadhiri wa UNFPA.
Akiongea na waganga
wakuu wa hospitari za Halmashauri ya Kahama na Msalala wauguzi
, idara za elimu za msingi na sekondari , maofisa maendeleo ya
jamii , Mkurugenzi Mtendaji wa KIWOHEDE Justa Mwaituka
alisema mradi huo utakuwa kwanza kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili
iweze kuwasaidia kujikinga na athari mbalimbali katika maisha yao.
Kwa upande wake
Muuguzi wa Hospitari ya wilaya anayeshughurikia mambo
ya afya ya uzazi Rehema Kantabula alisema Kahama
inakabiliwa na tatizo kubwa la watoto wa kike kupata ujauzito
na kuolewa katika umri mdogo ,
kukatishwa masomo hali ambayo imekuwa ikiwafanya
wasichana kuishi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na uelewa
juu ya maisha.
Kwa upande wake kaimu
mganga mkuu wa Halmashauri ya Msalala Nyembea Hamad alisema
swala la watoto wa kike kupata ujauzito katika umri mdogo inapofika mda
wa kujifungua wamekuwa wakipata matatizo makubwa hali inayopelekea
wengine kufariki wakati wa kuzaa na kuwa mradi
huo utasaidia kukabiriana na tataizo hilo.
Naye kaimu mganga mkuu
wa hospitari ya Halmashauri ya mji wa Kahama Heleni Membe alisema shirika la
UNFPA limeleta mradi huo kwa mda mwafaka kutoka na kuwa wilaya ya Kahama
inakabiriwa na tatizo kubwa la watoto wa kike kupata ujauzito katika umri
mdogo , kukatishwa masomo pamoja na wazazi , walezi kuwaoza
wasichana katika umri mdogo kutokana na uelewa mdogo juu elimu ya
afya ya uzazi.
Mwisho.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI