Baadhi ya vitanda vya wanafunzi vilivyookolewa baada ya Mabweni ya Sekondari ya Bupandagira kuwaka moto.
NI moja ya mabweni kati ya manne yaliyoteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu
BINTI Esta Mariko wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Bupandagira,akiwa katika hospitali ya Somanda wilayani Bariadi anakopatiwa matibabu baada ya kupata mshituko uliotokana na Bweni analoishi kuteketea kwa moto.
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Bupandagira;Mlambe Majani,akiwa ni mmoja wa majeruhi waliolazwa hospitali ya Somanda wakipatiwa matibabu,baada ya kunusurika kuteketea kwa Moto,ulioharibu samani na majengo ya shule hiyo.
WANAFUNZI;William China wa kidato cha tatu katikati akiwa na Williamu Ngembe wa kidato cha pili aliyeketi kushoto pamoja na Musa Jacobo wa kidato cha tatu wakiwa katika hospitali ya Somanda wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wakiwa wadini wameketi baada ya kupatiwa matibabu.
Ni moja ya athari iliyopatikana kutokana na hitilafu hiyo ya nishati ya umeme.
Pamoja na kuteketea kwa mabweni hayo,hivi ni vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi katika Shule ya Sekondari hiyo.
MOJA ya Mabweni ya Mkapa Hall A,B,C na D ambalo liliteketea na Moto unaosadikiwa ulitokana na hitilafu katika Umeme.
MOTO mkubwa umesababisha hasara ya Shilingi 81,430,000/= katika Shule ya Sekondari ya Bupandagira,ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu baada ya kuzuka kisha kuteketeza mabweni manne na kusababisha wanafunzi wanne kulazwa katika hospitali ya Somanda.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bupandagira;Clivate Otieno,alisema moto huo unaosadikiwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ulitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi wakiwa katika madarasa wakijisomea,na kuteketeza mabweni manne yaitwayo Mkapa A,B,C na D.
Alisema moto huo haukuleta madhara makubwa zaidi ya kuteketeza majengo na baadhi ya samani zake za ndani na kuwatia mshtuko baadhi ya wanafunzi ambao waliwakimbiza hospitali ya Somanda kupatiwa matibabu.
Mkuu huyo wa Shule hiyo aliwataja wanafunzi waliopatwa na mshituko kiasi cha kukimbizwa na kulazwa katika hospitali ya Somanda kuwa ni Malambe Majani,William China na Musa Jacobo wote kidato cha tatu,wengine ni Esta Mariko wa kidato cha nne pamoja na Williamu Ngembe wa kidato cha Pili.
Chanzo cha Habari ni Gabriel Muhindi wa Bariadi Mjini. KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI