Mshindi wa kwanza wa Shindano la Hesabu kwa Wasichana lililoandaliwa na HUHESO FOUNDATION;Doricas James Limbati,akimkabidhi zawadi ya vitabu mama yake mdogo;Aurelia Mathias Limbati,ambayo ilikuwa ni miongoni mwa zawadi alizokabidhiwa.
Kwa furaha kubwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo;Doricas James Limbati akikionyesha kitita cha Shilingi Laki Moja kwa wanafunzi wenzake,hawapo pichani.
MKURUGENZI wa HUHESO FOUNDATION ya mjini Kahama;Juma Mwesigwa mwenye kapero akimkabidhi zawadi ya Mshindi wa jumla,ambayo ni Mpira wa Soka,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Majengo;Masula Japhet Ngulu.
Mmoja wa washindi wa pili ambao walifungana watatu;Agnes Boniphace wa Shule ya Msingi Majengo akipokea zawadi ya kitita cha Shilingi Elfu Hamsini na vitabu kutoka kwa Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa,wanaoshuhudia tendo hilo ni mama mzazi wa Agnes,aitwae Leticia Buchuma mkazi wa Majengo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo;Masula Japhet Ngulu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kahama;Kapteni Mstaafu Robart Mabala,akimkabidhi msindi wa tano;Martha Sungulwa,zawadi yake ya Shilingi Elfu Ishirini.
Baadhi ya wazazi walioshuhudia utoaji wa zawadi kwa wasichana walioshiriki Shindano hilo.
MWENYEKITI wa Kamati ya Shule ya Msingi wa Kahama;Kapteni Mstaafu Robart Mabala,akimkabidhi zawadi miongoni mwa washindi wa pili ambao walikuwa watatu;Tatu Chatta kitita cha Shilingi Elfu Hamsini na vitabu.
Mmoja wa washindi wa pili;Cecilia Kishiwa wa Shule ya Msingi Busoka,akipokea zawadi yake ya Shilingi Elfu Hamsini kutoka kwa Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa,katika anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busoka;Andrew Katto.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyahanga A wakishuhudia utoaji wa zawadi kwa mshindi wa kwanza.Shindano hilo lilishirikisha wasichana 63 kutoka shule za msingi 15 kutoka katika Halmashauri ya Mji wa Kahama. KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI