Add caption |
Add caption |
Add caption |
Add caption |
Add caption |
Add caption |
VIJANA WAASWA KUTOKIMBILIA NDOA PASIPO KUFAHAMU
CHANGAMOTO ZAKE.
IMEELEZWA kuwa kuvunjika kwa
ndoa nyingi katika zama hizi zinavunjika na kusababisha kuwepo kwa wimbi la
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokana na Vijana wengi kuingia
katika maisha ya unyumba pasipo kujua changamoto zake.
Hayo yalielezwa na Mchungaji
Jacob Ochola wa Kanisa la African
Inland Church
la Majengo wilayani Kahama,katika Jubilei ya miaka hamsini ya ndoa ya Mzee
Mathias Mulela[77]na mkewe Esther Gombanila [69]wakazi wa Kata ya Majengo
katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mchungaji Ochola alisema
ongezeko la watoto la mitaani linachangiwa na wana ndoa kutengana,kitendo
kinachosababisha ukosefu wa umakini wa malezi ya watoto kutoka pande mbili za
wazazi hivyo kuwalazimu watoto kuingia mitaani na kuanza maisha yasiyo na tija na hatari kwa Taifa letu la baadaye.
Alisema kiini cha tatizo hilo ni kutokana na vijana
wengi kujitumbukiza katika maisha ya ndoa wakiwa katika umri ndoa lakini
wakijikuta wakifuata mkumbo wa kufunga pingu za maisha pasipo kuzifahamu na kujiandaa
kukabiliana na changamoto za ndoa.
Hivyo aliwaasa vijana
kutokimbilia maisha ya ndoa pasipo kufahamu changamoto zake ili kuepuka
kutoheshimiana ambacho kimekuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi na
kulinusuru Taifa kuwa na kizazi cha watoto wa mitaani ambao mazingira ya maisha
yao ni hatari
kwa maendeleo ya Nchi.
Aidha aliwapongeza bwana na
bibi Mulela kwa kufaulu kuvuka vikwazo vingi vya kimaisha ambavyo vingeweza
kusambaratisha ndoa yao,na
kusisitiza hiyo inatokana na wanandoa hao kuamua kufunga pingu za maisha huku
wakiwa wanatambua changamoto za ndoa na kukubaliana nazo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI