Friday, December 1, 2017

NYALANDU ATOA USHAURI UMOJA WA MATAIFA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

L
azaro Nyalandu,aliyejiuzuru uwakilishi wa Wananchi katika jimbo la Singida Kaskazini,ameushauri Umoja wa
Mataifa,kuchukua hatua dhidi nchi ya Libya kutokana ukiukwaji wa haki za binadamu zinazoendelea nchini humo.

Nyalandu aliyepata kuhudumu nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii kipindi cha serikali ya awamu ya nne,ameuomba Umoja huo hima  kuchukua hatua zaidi juu ya kinachoendelea nchini Libya.

Amesema kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kwa kile kinachoendelea nchini Libya ili kuweza kukomesha kile ambacho kinaendelea kwa sasa dhidi ya binadamu.

“Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika lazima uchukue hatua dhidi ya Libya sasa. tunachoshuhudia ni matusi kwa wanadamu,”amesema Nyalandu

Aidha, siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zikiripotiwa kutoka Libya kuwa kumekuwa na biashara ya utumwa ikifanyika ikihusisha Libya kuuza Waafrika nchi za Ulaya.

Ubalozi wa Libya nchini Tanzani umesema kuwa Waafrika wanaodaiwa kuuzwa kutoka nchi hiyo, yawezekana walikuwa wanakabidhiwa kwa watoroshaji ili wawapeleke Ulaya na sio kuwauza kama watumwa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI