J
|
eshi la Polisi
sambamba na wadau kutoka sekta mbali mbali jijini Mwanza wameelimishwa
kubadilisha mitazamo
yao juu vijana wa mitaani,kuwa ni jamii isiyowezekana
iliyotawaliwa na vitendo vya kiharifu.
Wameaswa kuondokana na fikra kwa vijana
wa mitaani kuwa ni jamii iliyoshindikana kimaadili na wanaokwaza jitihada za
kujikwamua kimaisha kwa baadhi ya watu, badala yake wawaone kuwa wana mitazamo
chanya ya kuleta maendeleo ya nchi,anaandika
Tunu Herman; Mwanza.
Afisa Mradi wa Shirika la Railway Children
Africa,Adamu Kaombwe,amesema jamii ina mtazamo hasi na vijana wa mitaani kiasi
cha kuwakatia tamaa,kitendo ambacho si cha kiungwana,na kutokana na kubaini
hilo shirika lake limeona ni vyema likaanzisha hamasa ya kuwathamini vijana
hao.
Amesema kuokana na jamii kutowathamini
vijana shirika lake likaamua kuwakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali
ikiwemo Jeshi la Polisi kwa lengo kuzungumzia changamoto zinazowakabili watoto
wa mitaani ambazo zimekuwa chanzo cha wao kutokukubalika katika
jamii.
Alisema kwa sasa, jamii imewatenga
kutokana na muonekano wao wa nje pasipo kujua ndani wanamalengo mazuri, hivyo
wakati umefika wa kuwathamini na kushirikiana nao katika fursa mbalimbali
zinazojitokeza.
“ Matumaini yangu ni kuwa
kupitia semina hii, kila mtu atakuwa na muonekano mpya na kuondoa
daraja lililopo mbele la utengano na kuweka umoja utakaoleta tija na
maendeleo ya nchi “alisema Kaombwe.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii
mkoa wa Mwanza Wambura Kizito alisema, ili kuleta usawa kati ya jamii na vijana
hao, ni vyema yakahamasishwa mabadiliko kuanzia muonekano wao wa
uvaaji,ili uwe wa staha.
Wambura amesema pia kuwahamasisha vijana
hao, kushiriki shughuli za kijamii pamoja na kuanzisha vikundi ambavyo
vinatambuliwa na serikali ili waweze
kupata mikopo pamoja na wale wenye watoto kuhakikisha hawaingii
mitaani.
Naye Prisca William mmoja ya watoto
waliokuwa wanaishi mitaani alisema wataitumia vizuri fursa hiyo
walioipata ya kukutanishwa na viongozi wa polisi na wadau kwani mwanga
uliopotea kwa muda mrefu umeanza kuonekana ambapo mwanzo walikuwa wanaona kila
mtu anayewazunguka ni adui kwao.
Alisema jamii itambue sasa nao
wanajitambua, wanajiamini na wana uwezo wa kufanya vitu ambavyo vinaweza
kukubalika na kuleta maendeleo hivyo washirikishwe kwa kila fursa
zinazojitokeza .
Hata hivyo Mkuu wa Polisi wa wilaya ya
Ilemela SSP Ndagile Makubi alisema, wanahitaji Tanzania
inayosaidia jamii na vijana wanaozingatia maadili na kutii sheria na kuacha
tabia ambazo siyo nzuri,kuepuka makundi mabaya, kushinda vijiweni na sehemu
zinazotiliwa mashaka sambamba na kufanya kazi halali.
Pia aliwaomba vijana hao kushirikiana
na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu, ili kuhakikisha tunakuwa na
taifa salama na lenye amani.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI