B
|
aadhi ya Watanzania wamejitokeza kupanda Mlima Kilimanjaro huku
wakitoa hamasa ya kuchangia sekta ya afya kwa lengo la
kusaidia uzazi salama
wakati wa kujifungua kwa wanawake.
Watanzania hao wamesaidia upatikanaji wa mashine
maalumu ya kutoa dawa za usingizi kwa mama wajawazito wenye uzazi pingamizi
wakati wa upasuaji kwaajili ya kuokoa maisha yao,na kuikabidhi serikalini.
Mashine hiyo wameikabidhi Serikalini kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo Jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya
Afya Mh.Ummy Mwalimu alisema kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kupambana
na vifo vya wakina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.
Waziri
Ummy alitoa pongezi kwa watu waliojitolea kupanda mlima Kilimanjaro kwa
ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto
wakiongozwa na Dkt.Ahmed Mohamed Makuwani.
Alisema kuwa
waliopanda mlima Kilimanjaro wamewezesha kupatikana kwa msaada wa
mashine hiyo, hivyo akawashukuru na kuomba wadau wengine kuiga mfano
huo.
“Tunawashukuru
Utepe Mweupe wa Uzazi Salama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya
katika kushirikiana na serikali ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi
na vifo kwa watoto wachanga, hatua hii inatufariji sana na naomba
watanzania na wasio watanzania wenye mapenzi mema na afya ya mama na
mtoto kuendelea kusaidia juhudi hizi ”, alisema Waziri Ummy.
Akieleza
mafanikio katika sekta ya Afya waziri Ummy alisema kuwa kuna zaidi ya
vituo vya afya 480 nchi nzima na kati ya hivyo vituo 109 vinavyumba vya
upasuaji ambayo ni sawa na asilimia 20 huku akibainisha kuwa kufikia
Juni, 2018 serikali inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji 170
vitakavyosaidia upasuaji wa mama wenye uzazi pingamizi na idadi hiyo
itaongezeka na kufikia vituo 279.
Aidha
Waziri Ummy alisema kuwa licha ya kujenga vyumba hivyo watahakikisha
upatikanaji wa vifaa, ujenzi wa maabara kubwa, wodi za kinamama pamoja
na nyumba moja ya mtumishi katika vituo vya afya vyenye vyumba vya
upasuaji.
Kutokana
na mpango mkakati wa kupambana na vifo vya wajawazito na watoto
wachanga Serikali inatarajia kufikia asilimia 50 mpaka asilimia 80
ifikapo mwaka 2020 ambayo ni kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayotarajia kuzinduliwa hivi karibuni ijulikanayo kama ‘Jiongeze
Tukuvushe salama’ kampeni ambayo inalenga kuwasaidia wakina mama
wajawazito popote walipo ili kuokoa maisha yao.
Naye
Mratibu wa Utepe Mweupe Dkt. Rose Mlay alisema kuwa mashine hiyo ni
maalum katika kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia inaweza
kutumika kwa mtu yeyote mwenye matatizo ya kufanyiwa upasuaji.
Kwa
upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alisema mashine hiyo iliyotolewa
na shirika la the Guardian Health yenye themani ya Shilingi milioni 55
ina ubora na kiwango cha kutosha katika kutoa huduma kwa mgonjwa wakati
wa upasuaji.
“Mashine
hii ni ya kipekee kwa sababu ina uwezo wa kutengeneza oksijeni na
haihitaji mitungi ya gesi kwa hiyo ni mashine nzuri kwa wagonjwa na
akinamama wenye uzazi pingamizi”, alisema Dkt.Mpoki.
Dkt.
Mpoki alisema kilichopo sasa ni kufundisha wataalam watakaohusika na
matumizi ya mashine hiyo ili waweze kuitumia ipasavyo na kuahidi kuwa
atahakikisha inatunzwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI