WABUNGE kutoka Vyama vya Upinzani katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wamefungua kesi
kutaka vikao vya Bunge vizingatie Kanuni
za kudumu.
Upinzani umeamua kufungua shauri hilo Mahakama Kuu Dodoma
wakiiomba mahakama itamke kuwa Spika ataliongoza Bunge kwa kufuata kanuni za
kudumu tu.
Hii ni baada ya Spika kumzuia John Mnyika kuhudhuria bunge kwa wiki moja
ambapo upinzani wamedai hakuna adhabu kama hiyo kwenye kanuni.
Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua
Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu
Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika.
Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu.
Hakuna kanuni inayosema Spika anao Uwezo wa kumfungia Mbunge siku saba.
Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI