
GOLIKIPA mahiri wa mabingwa wa soka nchini Dar Yanga African,Deogratias Munishi "Dida" ameitega klabu yake hiyo anayoichezea kwa kutokuwa tayari kusaini mkataba
Mkataba wa sasa wa Dida unaisha June 30 mwaka huu 2017.lakini kwa kipindi hiki hayupo tayari kuongea na timu yoyote ya hapa nchini ikiwemo timu myake ya Yanga hadi atakporejea na kutambua hatima ya majaribio anayopanga kuyatekeleza hivi karibuni.
Dida amejinasibu kuwa kiu yake kubwa kwa sasa,nikupata changamoto katika Klabu nje ya nchi,na si timu za hapa nchini,na kudai hayupo tayari kwa kipindi hiki kufanya maongezi yoyote na timu ikiwemo Yanga.
Hajasaini kwasababu anataka kwanza kwenda kufanya majaribio nje ya Nchi ndipo aamue kama atasaini au Hatasaini, kwani anakumbuka msimu wa 2015/2016 aliwahi kutakiwa na timu mmoja nje (Bidvest ya South Africa) lakini kutokana na mkataba aliokuwa nao Yanga ukamuwia vigumu kutoka Yanga.
Ndiyo maana anataka akomae kwanza akiwa hana mkataba na Yanga ili dili likitiki yeye ndiye awe mwenye maamuzi ya Mwisho, Ila alisema anashukuru kwasapoti anayopewa kutoka kwa wanaYanga KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI