CHAMA cha
Mapinduzi,kimevikebehi vyama vya Upinzani,kwa kujinasibu
Rais John Pombe Joseph
Magufuli,kasi ya utenda kazi wake unatokana na ilani ya chama hicho.
Kimedai hatua
alizochukua kuhusiana na makontena 277 ya mchanga wa dhahabu ( Makinikia
)yaliyodhibitiwa bandarini,ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho,na abadani hajapoka
sera za upinzani.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula amesema kitendo alichokifanya
Rais John Magufuli cha kuwafichua wanaotorosha mchanga wa madini kipo kwenye
ilani ya chama hicho hivyo wapinzani waache kudandia treni kwa mbele.
Akizungumza na wanachama wa CCM kwenye kongamano la kuunga mkono juhudi za Rais na kumpongeza kwa kuwafichua mafisadi,kitendo kinachofanya serikali yake inayoongozwa na CCM,kuzidi kuaminika na kujijengea msingi imara wa kuendelea kushika dola.
"Alichokifanya Rais kipo ndani ya ilani ya chama, wapo wanaotaka kudandia treni kwa mbele wakidai wao ndiyo walikuwa na mawazo hayo, nataka niwaambie Rais anatekeleza ilani hiyo ni mipango ya CCM, "amesema.
Pia, Mangula amewaonya watu wanaoibuka na kutaka kukwamisha kazi anayofanya Magufuli kuwa hawataweza na nchi haitashtakiwa kama wanavyodai.
“Niwatoe hofu wananchi na wanachama wote kuwa nchi iko salama zaidi tumuunge mkono Rais wetu kuwafichua wezi wa mali za nchi, "amesema .
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI