NASSIB
Abdul,almaarufu;Diamond Platinumz,mkali wa Bongo Fleva,ameurudia kwa umahiri
wimbo wa Maria Salome,uliompatia
umaarufu mkubwa,Saida Karoli.
Wimbo huo ;Maria
Salome,ulimuibua miaka ya 2000;Saida Karoli,kutokana na tungo yake maridhawa na
kuendelea kutoa tungo zingine zenye maudhui ya muziki wa asili,uliokuwa wa aina
yake,wenye miondoko ya Kabila la Wahaya,na kumpatia umaarufu,katika Ukanda wa
nchi za Afrika Mashariki,anaandika Tatu Mwinyi.
Mkongwe huyo wa nyimbo za
asili,katika enzi za kilele cha mafanikio,alikuwa katika uangalizi wa FM
Studio,chini ya Ukurugenzi wa Felician Muta,enzi zake zilionekana kufikia
tamati baada ya mvumo uliotikisa kila pembe,na kwa watu wa makabila yote nchini
na Afrika Mashariki,hata kusahaulika.
Lakini hivi
karibuni,Diamond Platinumz,kupitia lebo yake ya Wasafi Classic
Baby(WCB),wamemuibua na kumrejesha Saida Karoli,katika medani kwa kutumia wimbo
Maria Salome,wenye kibwagizo chenye msisimko cha;Chambua kama Karanga.
Diamond
Platinumz,ameucheza upya wimbo huo kwa kushirikiana na mmoja wa wasanii katika
lebo yake ya WCB,Raimond,kwa ruhusa na makubaliano na Saida,ambaye amekiri
kibao hicho kutendewa haki na vijana hao wa kizazi kipya.
Aidha msanii mahiri wa
kizazi kipya,Sara Kais “Shaa”,amepongeza kazi hiyo nzuri iliyofanywa na wasanii
hao kutoka lebo ya WBC,huku akidai kwa kipindi kirefu alikuwa na wazo la
kuufanyia remix wimbo huo,isipokuwa majukumu yalimkwamisha kuonana kwa wakati
na Saida.
Shaa anasema, “….Maria
Salome,upo kiafrika zaidi,nimefarijika Diamond kuurudia na ameutendea
haki,kadri fikra zangu zilivyokuwa zikinituma kuutendea.”
Hata hivyo amebainisha
kwamba baada ya wasanii wa WBC kumuwahi anafikiria kutoka kivingine kwa
kuangalia kitu kingine.