WAZAZI na walezi
nchini,wametakiwa kuhakikisha vijana wao wanapata elimu stahiki pasipo kuruka
hatua mojawapo ya masomo kwa kuepuka tabia inayofanywa na baadhi ya
jamii,kuwaanzisha elimu ya sekondari baada ya kujiridhisha vijana wao
wanaufahamu mzuri na lugha ya Kiingereza.
Mwito huo umetolewa maalumu
kwa Jamii ambayo ina watoto katika Shule za English Medium,na kuonesha ufahamu
mzuri wa kuongea Kiingereza,imeaswa kuondokana na tabia ya kuwaanzisha kidato
cha kwanza vijana wao kabla hawajahitimu elimu ya msingi,kwakuwa tabia hiyo
inachangia kuporomoka kwa elimu nchini.
Juzi katika mahafari ya 15 ya Shule ya Msingi ya
Kwema English Medium,iliyopo mjini Kahama na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi katika Serikali ya awamu ya Nne,iliyoongozwa na Rais Jakaya
Kikwete;Philipo Mulugo,kwa kulaani tabia hiyo na kuahidi kupambana nayo ili
kuitokomeza.
Mulugo ambaye kwa sasa ni
Mbunge wa Jimbo la Songwe,mkoa mpya wa Songwe,alisema wapo wazazi wakiona
watoto wao wanajua kuongea lugha ya Kiingereza vizuri wanawarusha kabla ya
kumaliza darasa la saba na kisha kuwaanzisha elimu ya sekondari,pasipo kutambua
kuwa kitendo hicho kinachangia kuporomosha elimu nchini.
“Lazima turejeshe heshima
ya elimu nchini,hili suala la kurusha watoto,nakwenda kulizungumzia Bungeni,nina
imani na Waziri wa Elimu,Professa Joyce Ndalichako,ni msikivu ataniunga mkono,lazima
tuwasake wanafunzi vilaza hao”alisema Mulugo.
Kabla ya hapo Mkurugenzi
wa Shule ya Kwema English Medium,Pauline Mathayo,alisema uendeshaji wa shule
hizo una changamoto nyingi pamoja na kufanya vizuri kitaaluma lakini wazazi
wakiishaona watoto wao wanaongea kiingereza vizuri huwakatisha masomo ya msingi
na kuwaanzishia ya sekondari hali ambayo siyo sahihi.
Mathayo alisema wazazi
waelewe kwamba elimu ya msingi ni kuanzia chekechekea hadi darasa la saba,hivyo
kumkatisha mwanafunzi akaishia darasa la tano au la sita na kisha kuanza
sekondari anakuwa hajamalimiza kusoma mitaala yote ya shule ya Msingi,hivyo
pamoja na kwamba anaweza kufanya vizuri sekondari lakini atakuwa amekosa vitu
vingi kwenye elimu ya msingi.
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule
hiyo ya Kwema English Medium,Ignatus Mutoka,alisema changamoto iliyopo kwenye
shule binafsi ni serikali kutowashirikisha kwenye mabadiliko ya mitaala hali
ambayo hubadirisha bila kuwapa elimu,hali ambayo huwapa muda wa ziada na wao
kujenga uelewa upya wa mitaala hiyo.
Mutoka alisema Serikali
imekuwa ikiwajali walimu wa Shule za Serikali peke yake kwenye mabadiliko hayo
ikiwemo kuwapa mafunzo huku ikiwatenga wa shule binafsi,wakati mtihani ni
mmoja hata yale mafunzo ya K,K.K ;Kuandika,Kusoma na Kuhesabu,walipewa mafunzo
walimu wa shule za serikali peke yao,hali ambayo ilipaswa kuwashirikisha walimu
wote.
Kufuatia hali hiyo,Mulugo
aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafari hayo,ambayo alitunuku Vyeti kwa wanafunzi
254,waliomaliza darasa la saba,kwenye shule alisema yote hayo waliyoyasema
atakwenda kuyazungumzia Bunge,huku akikiri kwamba Tanzania haina chuo cha
Ualimu,wa kufundisha walimu wa shule za English Medium,hali ambayo mafanikio
waliyonayo ni juhudi zao binafsi za kutafsiri,mitaala ya Kiswahili na kuiweka
kuwa ya Kiingereza.