NI
miezi minne imefika,tangu Rais wa awamu ya tano,John Joseph Pombe
Magufuli,ateue saufu yake ya Wakuu wa wilaya na kuacha baadhi ya wateule wa
mtangulizi wake;Jakaya Kikwete.
Wahenga
walinena;Kuvunjika kwa Koleo sio mwisho wa Uhunzi.Bali Mhunzi ni budi atafute
njia mbadala kukamilisha shughuli yake.Ndivyo ilivyo kwa Yahaya Nawanda,baada
ya kutokuwa tena mteule katika wadhifa wakuu wa wilaya aliyoutumikia katika
Serikali ya awamu ya nne,amejikita katika Ujasiriamali.
Nawanda
ambae katika serikali ya Awamu ya Nne kwa nyakati
tofauti alishika nadhifa hizo katika
wilaya za Singida,mkoani Singida na Kilindi mkoani Lindi,ameibuka na kudai
maisha yake kwa sasa ni ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Katika
Mkutano wa Fursa ulioandaliwa na Clouds Media Group, Septemba 8,mwaka huu mjini
Kahama,Nawanda alisema mpaka sasa ana miliki zaidi ya kuku 50,000 ambapo
alianza kwa kuku 32,baada ya kutokea kupewa kuku wawili akawatelekeza.
Aliwataka
vijana kuwa na mawazo ya kufanikiwa,kwani kama kutaonesha kukata tamaa basi
watambue hawataweza kufanikiwa,kwakuwa mafanikio yanapatikana kwa juhudi na
kuanza kwa kidogo,pamoja na kwamba mawazo yapo kwenye malengo ya kitu kikubwa.
Anasema
kila shughuli inapaswa kuwekewa thamani,huku akitoa mfano wa kuku mmoja ambaye
ni biashara ya haraka na uhakika katika
masoko,kwani ana uwezo wa kuingiza Shilingi Elfu Ishirini na gharama ya
kumtunza kwa miezi mitatu mpaka kuanza kuzalisha ni Shilingi 4800/-.
Aidha
Mkuu huyo wa wilaya wa zamani anasema tatizo la jamii ni kutojali ufugaji wa
kuku hasa kwakuwatelekeza wanapowafuga huku akitoa mfano wa wengi wao
wakiisha wafuga huwatelekeza bila kujua maisha yao na wanapopata wageni
huwatafuta nyumba hadi nyumba,kwa lengo la kuwachinja kwa ajili ya kitoweo.
Amewakumbusha
Wajasiriamali kuwa na tabia ya ufugaji wenye tija ambao ni biashara inayoweza
kusaidia kutoka kipato cha chini hadi cha juu kwakuwa pamoja na yeye kuacha
Ukuu wa wilaya hivi sasa maisha yake ya ufugaji wa kuku yamemuwezesha kuishi
maisha mazuri.
Pamoja
na kuwa na elimu ya PHD,lakini haishi kwa kutegemea hiyo anaishi kwa kutegemea
ufugaji ambao pia unaweza kufanywa na mtu yeyote ambaye hana elimu yoyote,hivyo
ni fursa sasa kwa vijana kuwa na uelewa kwa kuwaza mbele zaidi.
Kabla
ya hapo Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto,aliwataka vijana kutambua kwamba
fedha na elimu vitu viwili tofauti na kuwataka wale ambao hawakufanikiwa kusoma
wasikate tamaa kwani kuna maisha mengine nje ya elimu,na wale ambao
wamefanikiwa kusoma wasome kwa bidii,kwakuwa lengo kuu ni kuishi maisha mazuri.
Semina
hiyo ya fursa imefanyika mjini Kahama,na
kuhudhuriwa na watu mbalimbali,wakiwemo vijana kwa wazee ambao wengi wao
walionesha kuvutiwa na mafunzo hayo,ingawa yalifanyika kwa siku moja,lakini
yameonyesha kuwa na tija kubwa kwa wananchi wa Kahama.