Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama,Timothy Ndanya,ambaye
aliwakilishwa na Afisa Tarafa wa Kahama Mjini,Julius Chagama,wakati wa ufunguzi
wa kituo cha kibiashara cha Kampuni ya Orion Lubricants ya jijini Dar es salaam, kilichofunguliwa
mjini Kahama ambapo aliwaasa vijana kuchangamkia
fursa hiyo ya kujipatia ajira.
Chagama
aliwaomba vijana kuondokana na tabia ya kushinda vjiweni huku wakilalamika maisha
magumu,kwa kutumia fursa ya Kampuni ya Orion,kuchukua bidhaa zake na za
wawekezaji wengine kisha kujitumbukiza katika shughuli za ujasiriamali kwa
kupeleka vijijini katika Halmashauri za Msalala na Ushetu,hali ambayo itawaongezea
vipato kwenye maisha yao .
“Hakuna
sababu ya vijana kunung’unika maisha magumu huku hawafanyi kazi,changamkieni
fursa ya ajira iliyopo sasa kupitia wakala wa Orion kwa kusambaza bidhaa
hizo,maeneo kadhaa hususani za vijijini kutokana na Wilaya,yetu kuwa ni kubwa yenye Halmashauri
tatu,”alisema Chagama.
Aidha
changama alisema wilaya ya Kahama ni ya pili kitaifa kwa kukusanya mapato hivyo
mzunguko wa kibiashara ni mkubwa ukilinganisha na wilaya zingine hivyo vijana
wenye lengo la kuwa wajasiliamali wananafasi kubwa ya kufanikiwa kwa kutumia
fursa hiyo .
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Bwana ni Mwema, Charles Mbwega, ambaye ni
wakala wa kampuni ya Orion Mjini Kahama,alisema kampuni yake imejipanga
kuzalisha ajira kwa vijana wachapakazi,waaminifu ili kukuza uchumi wa wilaya ya
Kahama.
Mbwega
aliwakumbusha vijana kuwa mafanikio hayapatikani kwa kubweteka vijiweni,bali
wakabiliane na changamoto zilizopo kwa kuachana na uzembe wa kufanya kazi,hatua
itakayowasaidia kukabiliana na maisha kwa kuondoa umaskini na kuzidi kuifanya
wilaya ya Kahama kufanya vyema katika kuchangia pato la Taifa.