MABINGWA
wa soka nchini,Yanga African imeshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada
ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1 – 1 na timu ya Medeama kutoka nchini
Ghana,katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mabao
ya timu zote yalipatikana kipindi cha kwanza,ambapo Yanga African ilitumia
dakika moja tangu kuanza kwa mchezo,uliochezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar Es
Salaam,kujipatia bao lilipachikwa kimiani na Donard Ngoma,baada ya kupokea pasi
safi kutoka kwa Msuva.
Medeama
walisawazisha bao mnamo dakika 17 ya mchezo kwa bao,lililofungwa na Benard
Danso,aliyeunganisha vyema mpira wa kona akiwa mbele ya Bossou.
Katika
pambano hilo,Yanga walionekana kuishiwa maarifa kwa kufanya mashambulizi yasiyo
na malengo ambayo yaliokolewa pasipo na presha na mabeki wa Medeama,huku dakika
89 ya mchezo mabeki wake wakijichanganya,lakini Abasi Mohammed aliyebaki na kipa
Dida akishindwa kutumia nafasi hiyo kupachika bao.
Katika Dakika 65 ya mchezo,Hisia za Ushirikiana zilimuingia Simon Msuva,baada ya kwenda kuzozana na kipa wa Medeama akitaka mfuko wa kipa aliouweka ndani ya lango,auondoe.Lakini haikuwezekana na pambano liliendelea.
Katika Dakika 65 ya mchezo,Hisia za Ushirikiana zilimuingia Simon Msuva,baada ya kwenda kuzozana na kipa wa Medeama akitaka mfuko wa kipa aliouweka ndani ya lango,auondoe.Lakini haikuwezekana na pambano liliendelea.
Kikosi cha Yanga kilikuwa;
01.
Deo Dida
02.
Juma Abdul
03.
Oscar Joshua/ Haruna Niyonzima[72]
04.
Kelvin Yondani
05.
Vicent Bossou
06.
Mbuyu Twite
07.
Simon Msuva
08.
Thabani Kamusoko
09.
Donald Gnome
10.
Amissi Tambwe/Juma Mahadhi[76]
11.
Obey Chirwa
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI