PICHA ya Maktaba. |
IMEELEZWA
pamoja na mkakati wa Serikali,kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu, wanafunzi
wote nchini kuketi katika madawati,Shule ya Msingi ya Hussein Nasser iliyopo
wilayani Nyang’hwale,mkoani Geita,tatizo bado ni kubwa,kufuatia robo tatu ya
wanafunzi wake,kuendelea kuketi chini.
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo,Godfrey Malandi,alisema hayo wakati wa makabidhiano ya
madarasa manne yaliyojengwa na Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,uliopo wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga,ambapo alisema tatizo la madawati shuleni hapo ni kubwa
na jitihada za kumaliza tatizo hilo zinasuasua.
Mwalimu
Malandi alisema Shule hiyo ina wanafunzi 439,huku ikiwa na madawati 97,ambapo
miongoni mwake yakiwa yamekarabatiwa na kukiwa na upungufu wa madawati 120,hali
inayofanya wanafunzi zaidi ya nusu kuendelea kuketi chini.
Alisema
sambamba na changamoto hiyo shule yake inakabiliwa pia na ukosefu wa vyumba vitatu
vya madarasa huku walimu wakiishi eneo la mbali na shule kutokana na kutokuwa
na nyumba za walimu za kutosha.
“…tunakabiliwa
na upungufu wa nyumba tano za walimu,pia ukosefu wa huduma ya maji safi na
salama hatua inayosababisha wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo.”Alisema
Mwalimu Malandi.
Aidha
Kaimu Meneja wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,unaomilikiwa na Kampuni ya
madini ya ACACIA,Benedict Busunzu,alisema kutokana na kufahamu changamoto za
kielimu,umekabidhi miradi miwili yenye thamani ya Shilingi Milioni 550.kwa
serikali ya wilaya ya Nyang’hwale.
Busunzu
alisema uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,umetekeleza miradi hiyo
kupitia Mfuko wa ACACIA Maendeleo,wakiwa na imani itachangia juhudi za utoaji
wa elimu bora kwa wanafunzi.
Ameitaja
miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa madarasa manne ,katika shule hiyo iliyopo kijiji
cha Mwasabuka katika Kata ya Mwingilo,ambapo darasa moja likijengwa kwa
asilimia mia moja na mgodi,mengine mawili kwa nguvu za wananchi na mgodi huku
moja wakilifanyia ukarabati.
Aliendelea
kusema sambamba na hayo pia Mgodi umetekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba moja ya
mwalimu,yenye uwezo wa kuchukua familia mbili na matundu 12 ya vyoo.
Kaimu
Meneja huyo alikabidhi mradi wa Jengo la kisasa la maabara tatu za Sayansi kwa
Masomo ya Fizikia,Kemia na Bailojia katika shule ya Sekondari ya Nyijundu na kuwahakikishia
Mgodi kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo katika eneo linalozunguka
uwekezaji wao.
“Mgodi
kujenga miundo mbinu imara kama majengo,ni endelevu ambapo umejiwekea mkakati
unaotekelezeka kila mwaka katika kusaidiana na jamii zilizo jirani na Mgodi,kama
uwajibikaji wa Mgodi kwa jamii,lengo letu ni kufanikiwa pamoja na
jamii.”Alisema Busunzu.
nayozunguka
eneo hilo ione faida ya uwepo wa Mgodi,na kubainisha utekelezaji huo hauhusiani
na tozo la ushuru wa huduma unaostahili kulipwa katika wilaya hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale,Ibrahimu Marwa,alisema jamii ni vyema
ikajenga mahusiano mema kwa kushirikiana na Mgodi kuhakikisha unafanya kazi
zake kwa amani ili uzidi kuchangia maendeleo katika wilaya hiyo.
“…ni
pongezi za dhati zimfikie Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale,Mheshimiwa Hussein
Nasser, kwa jitihada za kufanikisha kuanzishwa kwa shule ya msingi ambayo imeboreshwa
na Mgodi,lakini nasi wananchi tuwahakikishie usalama Mgodi katika shughuli zao
ili tuzidi kunufaika nao.”Alisema Mkuu wa wilaya.
Alitumia
fursa hiyo kudai serikali ya wilaya itahakikisha agizo la serikali la
kuhakikisha wanafunzi hawaketi chini ifikapo Julai na kuuomba Mgodi uone
umuhimu wa kuhakikisha wilaya ya Nyang’hwale inaondokana na tatizo hilo.
Hivi
karibuni Mgodi wa Bulyanhulu umekabidhi Shilingi Milioni Mia
Nne(440,000,000/-)kwa taasisi ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya mradi wa kuboresha
huduma za afya katika Halmashauri ya Msalala,Wilaya ya Kahama,mkoani Shinyanga.