NI TAHARUKI!Iliyoukumba mji wa Kahama kwa masaa
manne, Baada Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga jana kuwasambaratisha kwa
kutumia mabomu ya Machozi na gari la maji ya washa wafuasi na
Viongozi wa Juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa
wakitaka kufanya mkutano wa hadhra kuzindua Opresheni Okoa Demokrasia.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa saba za
mchana katika kiwanja cha CDT kilichopo mjini Kahama,wakati viongozi hao wa
ngazi za juu wa Chama hicho waliopokuwa wakitaka kufanya mkutano wa kufungua
kampeni ya operesheni okoa demokrasi kanda ya ziwa,ndipo askari polisi wa
wilayani Kahama waliongezewa nguvu na wenzao kutoka Shinynga
walipousambaratisha mkutano huo.
![]() |
POLISI wakiingia eneo la Mkutano |
Katika tukio hilo pia ilishuhudia Viongozi wa
Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe magari yao
yakimwagia maji ya kuwasha baada ya kuingia katika Viwanja hivyo vya CDT tayari
kwa kuanza Mkutano wao huo,na kulazimika kuondoka ndipo askari kuendelea kutupa
mabomu ya machozi na kusababisha kuzua taharuki kwa wananchi wa eneo hilo.
![]() |
WANANCHI waliokuwa katika Mkutano wakiserebuka kwa kuwazomea Polisi. |
Baadhi ya vijana hawakuafikiana na vitendo vya
jeshi la polisi hivyo kuanza kuwarushia mawe,jambo lililosababisha miongoni
mwao kukamatwa,na askari polisi kuendelea kulitawala eneo hilo hadi mitaa ya
jirani kwa kumwaga maji washa na mabomu ya machozi,hatua iliyozidisha taharuki
kwa wakazi wa eneo hilo hususani Waislamu ambao walishindwa kuandaa Futari kwa
ajili ya kufuturu.
Tukio hilo pia liliathiri biashara mbalimbali zinazofanyika eneo hilo ikiwemo mama Lishe waliamriwa na polisi kuzifunga na kuondoka,vingine wakibaki watajua ni Chadema na watawashughulikia kwani wao wanachoangalia;"Hapa ni kazi tu,kusambaratisha kila kiumbe katika maeneo hayo"
![]() |
GARI la Polisi likiwa na askari likiingia eneo la Mkutano. |
Hata hivyo baada ya kutokea hali hiyo ya
sintofahamu katika Viwanja hivyo huku wananchi wakikimbia ovyo kuimbia mabomu
ya mchozi yaliyokuwa yakipigwa na Askari wa Jeshi la Polisi kutoka Wilayani
Kahama kwa kushirikiana na wale waliopo mjini Shinyanga waliokuja kwa ajili ya
kuongeza nguvu ili kusambaratisha mkutano huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya
tukio hilo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe alisema kuwa kitendo
walichofanyiwa na Jeshi la Polisi sio cha kiungwana na kuongeza kuwa taarifa za
kufanya Mkutano wao huo walikuwa nazo tangu jana na hiwezekani kuwazuia leo
kufanya Mkutano.
![]() |
GARI za Polisi zikiwa na askari eneo la Mkutano |
Mbowe alisema kuwa hawataacha kufanya mikutano
yao hiyo kwani haki ya kila Mwananchi kupata taarifa na kuongeza kuwa kwa sasa
Wanakaa vikao vya ndani kwa ajili ya kujadili suala hilo na ikibidi
watalifikisha Mahakamani kwa fujo walizofanyiwa.
“Kwa sasa hatuwezi kuongea kitu kwa undani zaidi
tupo katika vikao vya ndani kwa ajili ya kujadili tukio hilo na ikibidi
tutalifikisha katika vyombo vya sheria kwa ajili ya kutolewa maamuzi kwa undani
kwani kila c chama kina uwezo kufanya mikutano ili mradi wafuate sheria”
alisema Mbowe.
![]() |
KATIKA uwanja wa Mkutano wananchi wakizomea polisi |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Mika Nyange
amethibitisha kutoa kwa tukio hilo na kuongeza kuwa walisitisha Mkutano huo
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zile za kiintelejensia ambazo waliokuwa
nazo kuhusu Mkutano huo kuwa kungetokea
machafuko na kulikuwa na makundi yaliyokuwa yamejipanga kufanya vurugu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI