Na Rajab Rachi.
MSANII wa Mduara,Snura
Moshi,ambae video yake ya wimbo Chura ilizua gumzo mitaani na kwenye mitandao
yakijamii amekiri kuteswa na wimbo kabla ya kufungiwa.
Snura aliomba radhi kwa
serikali na watu wote waliokwazwa nao,nakuahidi kutorudia tena kosa hilo kufuatia
jamii kumtafsiri kuwa ni mhuni aliyekithiri kufuatia wimbo wake wa Chura.
Alisema hakuwa na dhamira
mbaya ya kuipotosha jamii hata kufikia kumbeza na kueleza umempa funzo na kuahidi
kuwa balozi kwa maadili kwa wasanii wengine.
Snura alisema wimbo huo
kusimamishwa na serikali kwa kukiuka maadili sambamba na kutojisajiri Baraza la
Sanaa la Taifa {Basata}
lakini siku hiyo hiyo {Mei 4} aliyosimamishwa alikwenda kujisajiri na
kukumbushwa taratibu zote hivyo yupo huru kufanya sanaa.
Amesema
ataulekebisha wimbo huo na kuendelea kuutumia,Huu ni wimbo wapili kufungiwa
ukitanguliwa na Umevurugwa ambao pia ulifungiwa