NI pigo tena katika tasnia ya Maigizo nchini baada ya Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah "KINYAMBE" kufariki dunia leo usiku huko nyumbani kwao Mbeya.
Mmoja
wa wanandugu wa Kinyambe amethibitisha kuwa msanii huyo wa filamu
ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya
kuugua kwa siku kadhaa, ingawa bado haijafahamika ugonjwa aliokuwa
akiumwa.
Mchekeshaji huyo
ambaye alikuwa akishiriki katika filamu mbali mbali za ucheshi alianza
kuonekana kupitia kituo cha televisheni cha Chanel TEN katika kipindi
cha vituko show.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI