TAASISI ya kuzuia na Kupamba na
Rushwa(Takukuru)Mkoa Maalumu wa Kahama,inaifanyia uchunguzi miradi minne ya
maendeleo wilayani Kahama,ukiwemo wa jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari
ya Nyihogo,lililotelekezwa kwa kipindi cha miaka saba.
Akiongea na Waandishi wa Habari
Mjini hapa Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa maalumu wa Kahama Owen Jasson alisema
kuwa taasisi yake imekagua jumla ya miradi 11 ya maendeleo Wilayani
hapa ili kubaini kama taratibu za manunuzi zilifuatwa ikiwa ni
pamoja na wazabuni waliopewa kazi hizo kwa lengo la kubaini ikiukwaji wa
taratibu na matumizi ya fedha.
Jasson Alisema kuwa Pia
walikagua miradi hiyo ili kujiridhisha na kuona maendeleo ya Mradi husika na
pia kuona kama gharama ziliztumika katika kutekeleza miradi hiyo ilikuwa ni
sahihi na zinaendana na kazi iliyofanyika hali ambayo itachangia katika kuziba
mianya ya Rushwa iliyopo.
Aliitaja baadhi ya Miradi
waliotembelea kuwa ni pamoja na Mradi wa Maji, mmoja, Sekta ya Elimu miradi
mitano, Afya miradi miwili, Madini miradi mitatu, na kuongeza kuwa kwa upande
wa Elimu mradi mmoja uliokaguliwa ulikuta umetelekezwa kwa muda wa miaka
saba ambao ni wa jengo la Utawala la Shule ya sekondari ya Nyihogo.
Pamoja na mambo mengine Kaimu
Kamanda huyo alisema kuwa pia taasisi yake hiyo kwa kipindi cha mwezi
January hadi March 2016, Vilabu vya wapinga Rushwa viwili vimeimarishwa kwa
kuwakumbusha Wanafunzi juu ya wajibu wao katika mapambano dhidi ya Rushwa
pamoja na kupokea Wanachama wapya.
Hata hivyo alisema kuwa jumla ya
machapisho 245 yalisambazwa kwa Wananchi na kuongeza kuwa semina
mbalimbali pia zimefanyika kwa kuhusisha Walimu wa shule ya
Sekondari na Wanafunzi sambamba na vikundi mbalimbali vya wasanii
pamoja na makundi mbalimbali ya Dini.
Kuhusu Kesi Kaimu Kamanda huyo
alisema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi marchi mwaka huu
kulikuwa na jumla ya kesi sita zilizokuwa zikiendeshwa Mahakamani
ambapo nne ni za kipindi cha nyuma yaani kabla ya Januari 2016 na
kuongeza kuwa kesi moja kati hizo ilitolewa hukumu mwezi februari mwaka huu na
walishindwa kabla ya kukata rufaa kwa kuwa hawakuridhika na hukumu hiyo.
Katika suala la mazingira Kaimu
Kamanada huyo alisema kuwa kazi iliofanyika ni kufanya utafiti kuhusiana na
mianya ya Rushwa katika usimamizi na ukaguzi wa usafi wa mazingira
,kuandaa kikao cha Wadau kitakachofanyika mwezi aprili mwaka huu
kitakachowahusisha baadhi ya Watendaji wa kata, baadhi ya maafisa Afya kata,
Mkuu wa idara ya afya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji pamoja na Maafisa
wa TAKUKURU.