RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,jana ameibuka katika staili ingine baada ya kuvamia tawi la Benki ya CRDB (Holland Branch),la Jijini Dar Es Salaam,akiwa kwenye gari lenye namba
za usajili;T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya “Adamu na Hawa” wala bendera ya
Rais,kitendo ambacho kimesababisha kuzusha mjadala.
Rais Magufuli alifanya kitendo hicho kisichotarajiwa,katika Tawi la benki hiyo ambayo ipo makutano ya barabara za Ohio na Samora, katika Tukio hilo lililochukuwa dakika
25,ambalo limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam.
Mara baada ya Rais Magufuli
kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya barabara hizo
yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki
hiyo.
![]() |
Rais Dk. Magufuli akipunga mkono alipokuwa akiondoka
|
Wakati akikaribia kuingia ndani
ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki
hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao
waliyokwishaingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani
baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa
huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile.
Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote
waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva
wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya
kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli
akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea
ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua
tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo
kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa
inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha
kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema
Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi
wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua
wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa
ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi wakati Rais Magufuli
anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla
kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI