BAADA ya kimya cha muda mrefu,Mbunge
wa Jimbo la Kibamba,jijini Dar Es Salaam,John Mnyika,ameibuka na kumtaka Rais
John Magufuli,ahuishe Mchakato wa Katiba Mpya kwa kurejesha maoni ya wananchi.
Mnyika anasema,Rais Magufuli,anapaswa kuyafanyia
kazi maoni ya wananchi yaliyokusanywa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,
Jaji Mstaafu, Joseph Warioba,na si kubeba maoni yaliyotolewa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Anasema kuwa, Rais Magufuli anapaswa
kujua kwamba, ni jambo la msingi na busara kuheshimu maoni ya wananchi kwa kuwa
wao ndio wanaopaswa kuamua hatma ya taifa lao.
Awali Mnyika aliitoa kauli hiyo siku
mbili zilizopita wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Wanasheria -Justice Voices
Tanzania (JVT) unaoshirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UDI).
Kwenye uzinduzi huo Mnyika amemtaka
Rais Magufuli na Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria kutangaza siku
ambayo Mchakato wa Katiba Mpya utaanza na kwamba, irejeshe rasimu ya Jaji
Warioba.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI