Thursday, April 14, 2016

NAPE ACHARUKA,AIBUA MADUDU UWANJA WA TAIFA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye amekifunga mara moja kiwanda kilicho kuwa kikiendeshwa kwa njia zisizo halali na Wakandarasi wa Uwanja wa Taifa, Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China.

Kutokana na kusitishwa kwa karakana hiyo kumeifanya hatima ya Meneja wa Uwanja wa Taifa,Rish Urio kuwa shakani,kunakosababishwa na mazingira ya uwepo kwa karakana hiyo.

Nape alifanya zoezi hilo jana baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya Uwanja wa Uhuru “Shamba la Bibi” na kubaini kuwepo kwa kiwanda hicho ambacho ni kinyume na taratibu na mkataba wa kisheria walioingia baina ya Serikali na Kampuni hiyo ya Wachina kuhusu ujenzi wa miudombinu ya michezo pekee ikiwemo Uwanja wa Taifa na Uhuru.

Kabla ya kukifungia kiwanda hicho Waziri Nape aliomba maelezo ya kina juu ya uhalali wa uwepo wake na namna uendeshwaji wake unavyofanyika ili kujiridhisha ndipo alipofikia uamuzi huo wa kukifungia baada ya kujiridhisha kuwa kinaendeshwa kinyume na utaratibu.

Waziri Nape aliyefika uwanjani hapo saa 3:35 asubuhi,akiongozana na ujumbe wa wizara na Mshauri Mkuu wa Mradi huo,Aloyce Mushi,alitaka kujua kwa undani zaidi uhalali wa kiwanda hicho  cha useremala,ambacho kinakadiriwa kuwa na watumishi zaidi ya 15 kama kipo ndani ya mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na eneo changamani la michezo.

Uwepo wa kiwanja hicho kunapelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa maboresho na ujenzi wa Uwanja wa Uhuru.

Aidha Waziri Nape amemuagiza Meneja wa Uwanja wa Taifa Rishe Urio kutoa maelezo ya kina juu ya uwepo wa Kiwanda hicho katika eneo la ndani ya masaa 24 ni kwanini akutoa taarifa juu ya uwepo wa shughuli za Kiwanda hicho katika eneo hilo ila hali yeye ndiye msimamizi mkuu wa Uwanja huo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya BFG Cheng Longhai amekiri kuwa Kiwand hicho kinaendeshwa kinyemela kwakuwa hakihusiani na mkataba wa kampuni hiyo.

Wakatihuohuo Nape ameuagiza uongozi wa Selcom Tz kuhakikisha inakimilisha mfumo wa Tiketi za Kielekroniki na kukabidhi kwa Serikali ndani ya siku 30 kuanzia sasa.

Agizo hilo ni muendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim wakati akiongea na wadau wa sekta ya michezo kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu.

Waziri huyo anataraji kufanya ziara ya siku moja mkoani Shinyanga kesho,ambapo majira ya saa nane mchana atakutana na waandishi wa Habari wa mkoa huo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI