Saturday, April 9, 2016

MAALIM SEIF KUFUNGUKA KESHO HATIMA YAKE KISIASA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



BAADA ya kupatikana kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika uchaguzi wa marudio uliompa ushindi Dkt.Ali Mohammed Shein
(CCM),Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad,kesho kutoa mwelekeo wake na chama chake  kisiasa.

Katika kuelezea mwelekeo wake kisiasa pia anatarajia kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu,huku Dk.Shein akiwa ameishatangaza baraza lake la Mawaziri linalounda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea  urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.


CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.


Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.


Taarifa toka ndani ya chama hicho zilieleza katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu, ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, likiwemo la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi wa marudio.

 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI