NAIBU Waziri Ofisi ya
Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina, ameugiza uongozi wa Hospitali
ya Rufaa, Mkoani Iringa kulipatia ufumbuzi haraka suala la uteketezaji wa taka
ngumu katika hospitali hiyo.
Mpina alitoa agizo hilo jana
alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa,ikiwa ni ziara yake ya
kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira
katika viwanda, viliyopo katika mkoa wa Iringa.
Awali ilifahamika kwamba uteketezaji
wa taka hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa,umekumbana na changamoto nyingi
ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa
muda mrefu,pasipo kuwepo jitihada za matengenezo ama taratibu za utekelezaji
manunuzi serikalini.
Kwa Upande wake Mganga Mkuu
Mfawidhi wa hospital hiyo, dkt Robert Salim,alimueleza Naibu waziri huyo kuwa
taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la
mkoani hapo.
Dkt.Salim alisema kuwa hosptali
hiyo imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za
sindano, gloves, nyembe na bandeji maana haziozi ardhini kirahisi,kutokana na
kuharibikiwa na kifaa cha kuteketeza taka hizo.
Akitolea ufafanunuzi
sualala za uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya
nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw.
Godlove Mwamsojo,alieleza kuwa baraza limewahi kutoa ushauri kwa uongozi wa
hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao cha Sao
hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina vifaa vya kutosha.
Hata hivyo ushauri huo
haukuleta tija sana kutokana na kwamba
hospital hiyo huzalisha taka nyingi,hivyo kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia
kuziharibu.
Wakati huo huo, Naibu
Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika
usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo alipanda mti katika
kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa
taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha aliwaasa watunze
vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem cha
Kitwivu,huku akisisitiza umuhimu wa jamii kupanda miti ili kuepuka changamoto
za mabadiliko ya tabia nchi.
Naibu Waziri huyo
aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja
na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini
na tano kwa mwaka.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI