![]() |
ZUWENA Senkondo akimkabidhi Neema Mhoja vifaa vya Ukunga. |
WANAWAKE wajawazito katika Kata ya Mwingilo,wilayani Nyangh’wale mkoani Geita,huenda wakapata ahueni ya kujifungua salama kwa kuondokana kuhudumiwa na wakunga wa jadi,baada ya Mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama kutoa vifaa vya kujifungulia katika zahanati yao.
Akipokea
vifaa hivyo, Mratibu wa huduma ya Baba,mama na mtoto katika Halmashauri ya
Nyangh’wale,Neema Mhoja,alisema vifaa hivyo ambavyo ni seti nane,vyenye thamani
ya Shilingi Milioni tatu vitawasaidia uzazi salama akina mama wajawazito katika
eneo hilo na kuepusha vifo vinavyozuilika.
Awali
Muuguzi katika zahanati hiyo ya Mwingilo,Consatine Matata,alisema vifaa hivyo
vitaondoa tatizo la akina mama kujifungulia majumbani ama kukimbilia kwa
wakunga wa jadi,kutokana na zahanati hiyo kutokuwa na vifaa vya kutosha kutumia
wakati wa kujifungua.
“Akina
mama walikuwa wakishindwa kufika zahanati kujifungua,nasi kuwa na wakati mgumu kuwapatia
huduma kutokana na kutumia kifaa kimoja,ililazimika
kusubiriana baada ya kutumika kukichemsha
ndipo kutumika tena,hali hii iliwakatisha tama wengi wao kuja kujifungulia
Zahanati,”alisema Matata.
Kabla ya
hapo Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya
Acacia,Elias Kasitila,alisema waliamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la
kuimarisha ujirani mwema baina ya Mgodi
huo unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,uliopo wilayani Kahama na kata hiyo iliyo
wilayani Nyangh’wale.
Alisema
mbali ya kudumisha mahusiano ya ujirani
mwema,pia wanazingatia kuwa wanawake wajawazito afya zao ni nguzo ya msingi wa
maendeleo katika taifa,hivyo wanapaswa kulea mimba zao na kuwaandalia mazingira
bora yatakayowafanya wajifungue salama.
Aidha Kasitila
alisema walitoa vifaa hivyo baada ya kupokea maombi ya wananchi wa vijiji vya
Iyenze na Mwasabuka katika kata hiyo ya Mwingilo,ambao walielezea athari
zinazowapata wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua. Vifaa vilivyokabidhiwa
vina thamani ya Shilingi Milioni Tatu, vilitolewa katika zahanati ya