![]() |
WAZIRI wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi;Dkt.Joyce Ndalichako. |
Katika kikao cha wazazi
katika shule hiyo,kilibaini Mwenyekiti wa kamati ya Shule, Simon Soka,pamoja na
Mwalimu Mkuu wake, Lilian Lotasorwaki,walibainika na
tuhuma za kutumia vibaya fedha za wazazi
zaidi ya Shilingi Milioni tatu.
,kwakufanya ufisadi wa
zaidi ya shilingi milioni tatu wameanza kurejesha fedha hizo .
Akiongea na Tanzania Daima,Diwani wa
Kata ya Nyihogo, Shadrack Mgwabi,alisema wiki iliyopita wazazi walibaini
matumizi mabaya ya fedha walizochanga kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo
hivyo kuchukua maamuzi ya kuwazuia kuendelea kufanya kazi katika shule hiyo huku wakiagiza
fedha hizo kurejeshwa.
Mwenyekiti wa Shule hiyo,Soka,alisema
maagizo ya wazazi hayo wameanza kuyatekeleza kwa kuanza kurejesha fedha hizo,huku
akikanusha kuhusika na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa madai alizitumia ikiwa
ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake.
Hata hivyo pamoja na Soka kukanusha
tuhuma hizo,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Lotasorwaki,alimtwisha mzigo Soka
akimtuhumu kumlazimisha ampe fedha hizo hali ambayo iliwafanya wazazi
wawashutumu wote wawili kuhusika na matumizi mabaya ya fedha hizo.
Awali Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata
ya Nyihogo,Simon Mabumba, alisema watuhumiwa hao katika mkutano wa wazazi
wametuhumiwa kutumia fedha hizo kinyume na taratibu ambazo wazazi walichanga
kwa ajili ya kununulia matofari .
Mabumba alisema katika mkutano huo
wazazi hao walimvua madaraka Mwenyekiti
huyo wa shule ya msingi Kilima A huku wakitaka
hatua kali zichukuliwe dhidi ya wote hao wawili ambao wamehusika na upotevu wa
fedha hizo.
Kufuatia hali hiyo wazazi hao
walipitisha maazimio kwenye kikao hicho cha kuwachukulia hatua za kisheria
viongozi hao wa shule hiyo ambao sasa kwa mujibu wa diwani Mgwabi juzi tayari
walianza kurejesha kiasi cha shilingi milioni mbili na fedha zilizobaki
wanaendelea kuzilipa.