Sunday, December 6, 2015

MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI HAYAVUNJI SHERIA YA MANUNUZI "SEFUE"

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

 

KATIBU mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kutaka fedha zilizokuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima, kupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, hayavunji sheria ya manunuzi wala utaratibu mwingine wa kisheria.
 
Ufafanuzi huo aliutoa kwa kufahamisha kuwa lengo kubwa ni kusukuma maendeleo kwa kasi na katu haujakiuka sheria za manunuzi.
 
Hivi karibuni,Rais Magufuli aliagiza sh.milioni 225 zilizokuwa nimechangwa kwa ajili ya hafla ya wabunge zipelekwe Hospitali ya Muhimbili kununua Vitanda na Mashuka.

Aligiza pia Bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sherehe za Uhuru Disemba 9 zitumike kupanua barabara ya Mwenge- Morocco.

Akitoa ufafanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco, Balozi Sefue  amesema mradi huo sio mpya na kwamba taratibu zote zilishafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwalipa waliokuwa wamejenga  kando ya barabara.

Amesema kilichokuwa kinakwamisha mradi huo ni  pesa.

Akizungumzia sakata la wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyima likizo wafanyakazi huku wengine  wakitiwa rumande kwa masaa  6, Balozi Sefue  amesema serikali haina taarifa rasmi hivyo akalitaka shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kuwasilisha malalamiko serikalini badala ya kuishia kulalamika katika vyombo vya habari.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI