Thursday, December 24, 2015

KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI NI SIKU YA USAFI NCHINI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



KATIKA kuhakikisha inadhibiti magonjwa ya milipuko inayotokana na kukthiri kwa uchafu,Serikali imeamua kutangaza rasmi; kila Jumamosi ya mwisho
wa mwezi kuwa siku ya usafi Nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina, kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana; January Makamba.

Naibu Waziri huyo alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanikisha jambo hili na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kila siku.

Alisema suala hilo la usafi kuwa endelevu kwa kuwaagiza Wakurugenzi Watendaji katika Halmashauri za Manispaa,Miji na wilaya,kuhakikisha wanafanikisha zoezi hili kwa kuwaongoza wanaowaongoza kulifanya zoezi hilo kwa ufasaha.

Alisisitiza kuwa Serikali itawawajibisha mara moja,watendaji watakaozembea na kushindwa kusimamia zoezi hilo.

Aidha Waziri Mpina alisema kila mwananchi itamlazimu kuwajibika siku hiyo,kwa kufanya usafi katika eneo lake ili kuhakikisha mazingira yake yanaondokana na urafiki wa kukaribisha magonjwa ya milipuko.

Zoezi rasmi linaanza jumamosi ya mwisho January 2016.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI