![]() |
SIKU Rais Dkt.John Pombe Magufuli alipoongoza Watanzania kufanya Usafi. |
HALMASHAURI ya wilaya ya Masumbwe imeshindwa kutekeleza ipasavyo zoezi la usafi lililofanyika nchi nzima 9 Desemba Mwaka huu,baada ya kutekeleza zoezi hilo kwa kukusanya uchafu na kushindwa kuuhifadhi ipasavyo,badala yake umeutelekeza Kijijini Shenda katika Kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita na kusababisha wanakijiji hicho kuingiwa hofu kuibuka magonjwa ya mlipuko wa magonjwa kupitia uchafu huo.
![]() |
BAADHI ya Wakazi wa Kijiji cha Shenda wakishangaa Uchafu. |
Kufuatia hali hiyo,ambayo imetafsiriwa na baadhi ya Wanakijiji hao
kama ni kumchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,aliyeagiza kumbukumbu za Uhuru wa Tanganyika kuzitumia kwa kufanya usafi nchi nzima,hivyo kuitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka
zilizowekwa kijijini kwao.
![]() |
WANAKIJIJI cha Shenda wakistaajabu Uchafu. |
Wakiongea
na waandishi wa habari za mtandaoni wanakijiji hao wamesema kuwa
wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutuma takataka katika
kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.
Wameongeza
kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule
ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya
kuzuka kwa magonjwa ya mripuko,kutokana na taka hizo kuanza kuoza na kusambaa
katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.
![]() |
BAADHI ya Wanakijiji cha Shenda wakishangaa Uchafu. |
Sambamba
na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya Mkurugenzi kutupa taka hizo katika
kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika
kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kwa kutoa
harufu mbaya zinazoambatana na funza.
Kwa
mujibu wa Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Shenda, Joseph Jaseda, amesema sehemu
zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo
waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika hivyo kulazimika kutupa taka hizo katika maeneo hayo.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Masumbwe, Shimo Kiyuyu amesema kuwa alifikisha
malalamiko ya wananchi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe,akatoa gari ili uchafu
uzolewe lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na gari hiyo kwenda eneo
la uchafu bila wazoaji wa taka hizo.
Kwa
upande wake Afisa Afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe,Edward Razalo,amekiri
uchafu huo kutupwa katika maeneo hayo na kuongeza kuwa baada ya wananchi
kulalamika walienda kuweka dawa ya kuuwa wadudu katika taka hizo na kwamba
hawajazihamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.