ADHA
za wachimbaji wadogo kufunikwa na vifusi katika migodi wanapokuwa katika
shughuli za kutafuta mali,huenda ikapungua
kutokana na Chama cha wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga “SHIREMA”,kuanza kutoa Elimu ya uchimbaji salama kwenye migodi yake.
kutokana na Chama cha wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga “SHIREMA”,kuanza kutoa Elimu ya uchimbaji salama kwenye migodi yake.
Mkaguzi
mkuu kutoka chama hicho,Amos Mbaga,amebainisha hayo jana alipoongea na CGFM,kwa
kueleza kuwa timu ya Wataalamu wa Uchimbaji salama kutoka SHIREMA,imeanza kuzunguka
migodi yote kutoa Elimu hiyo.
Amesema
wameona umuhimu wa kutoa Elimu hiyo,baada ya mapema mwezi uliopita,Machimbo
katika mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama kutitia na kuwafunika wachimbaji
zaidi ya 11 ambao wengine waliokolewa na kubaki watano ambao baadaye
waliokolewa baada ya kuishi ardhini kwa siku 41
Hata
hivyo Elimu hiyo imekuja baada ya mkaguzi mkuu kutoka wizara ya nishati na
Madini Ally Samaje kuagiza migodi yote imarishwe ili wachimbaji hao wachimbe
kwa usalama zaidi
Samaje
ambaye alikuwa mjini Kahama akimuwakilisha Kamishina wa Madini Tanzania
amewataka viongozi wote wa chama hicho pamoja na wa migodini kutoa Elimu ya
usalama wakati wa uchimbaji madini kwenye machimbo hayo