HALMASHAURI za Ushetu na Msalala,zimeshutumiwa
kuchangia kuzorota kwa kilimo cha zao la Pamba katika wilaya ya Kahama,kutokana
na kuchukua ushuru huku wakishindwa kuboresha miundo mbinu ya barabara kuelekea
vijiji vinavyolima zao hilo.
Shutuma hizo zilitolewa na
Chama cha Wakulima wa zao la Pamba
Tanzania“TACOGA”Tawi la Kahama,ambapo kilisema katika kipindi hiki cha masika
miundo mingi ya barabara imeharibika na kutopitika,hivyo kusababisha pembejeo
za zao hilo kutofikishwa kwa wakati.
Akiongea na Tanzania
Daima,Katibu wa Tacoga wilaya ya Kahama,Paul Ntelya,alisema suala la miundo
mbinu ya barabara kuwa mibovu,nayo inachangia kuzorota kwa zao hilo wilayani
Kahama,kutokana pembejeo kutofika kwa wakati katika kipindi hiki ambacho
barabara zimeharibiwa na mvua.
“Mvua zimeharibu
barabara,baadhi ya makampuni ya wanunuzi wa zao la Pamba,walipeleka mbegu kwa
wakulima,lakini gari zao zimezama kabla hazijaenda kituo kingine kupeleka
mbegu,msimu wa masika nao hausimami matokeo yake watapanda kipindi kimepita
matokeo yake ni kutopata tija katika zao hilo,”alisema Ntelya.
Alisema Halmashauri hizo
zimekuwa mstari wa mbele kuchukua ushuru wa zao hilo huku ikishindwa kuboresha
miundo mbinu hiyo ambayo ni muhimu kwa usafirishaji wa pembejeo na zao hilo
kulifikisha sokoni kwa wakati kitendo ambacho hakiwatendei haki wakulima na
kuwafanya kukata tamaa ya kuzalisha zao hilo kwa wingi.
Aidha Katibu huyo alitoa
ushauri kwa Serikali kufuta ushuru huo na kuongeza katika Bei ya zao la pamba
ili mkulima anufaike jambo litakalomtia hamasa zaidi katika kuboresha kilimo
chake huku akihamasika kuchangia shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo inayoibuliwa na wananchi
wenyewe katika vijiji vyao ikiwemo ujenzi bora wa barabara.
Katika hatua nyingine Mbunge wa
Jimbo la Ushetu,Elias Kwandikwa,aliwataka wakandarasi wote watakaopewa na
Halmashauri kwa ajili ya kufanya kazi katika jimbo analoongoza kuhakikisha
wanaweka wazi mikataba yao kwa wananchi sambamba na kuonesha mpango kazi wao unapoanzia na
unapoishia,ili kuondoa walakini kwa wananchi.
Kwandikwa alisema hatua hiyo
itasaidia ujenzi imara wa miundo mbinu itakayokuwa na tija kwa wakulima wa
maeneo ya vijijini na hivyo kusaidia kuinua kipato cha mkulima kwa kupata
pemebejeo na kuuza mazao kwa wakati na kusaidia kuinua uchumi wa nchi.