Tuesday, November 10, 2015

SHILINGI MILIONI 143.2 KUTUMIKA KUANZISHA VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA KAHAMA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

SHIRIKA la The Foundation For Human Health Society “HUHESO FOUNDATION”la wilayani Kahama,linatarajia kutumia Shilingi Milioni 143.2  
 kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya kuweka na kukopeshana pesa kwa watu wenye vipato duni ili kuwajengea mitaji imara na kuwakomboa kimaisha.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION,Juma Mwesigwa,katika kikao cha Wadau kupitia Mradi wa Pesa kwa wote “PKW”ambao unalengo la kumkomboa mwananchi mwenye kipato duni kijijini amudu kujiwekea pesa katika Kikundi kisha kukopa kwa riba nafuu.
Mwesigwa alisema mradi huo wa Pesa kwa wote unaotekelezwa na shirika lake baada ya kupata ufadhili kutoka Care International,unatarajia kutumia kiasi hicho cha pesa kwa kipindi cha mwezi Julai 2015 hadi Juni 2016 katika vijiji vilivyo wilayani Kahama.
Alisema mradi huo wa pesa kwa wote watautekeleza kwa kipindi cha miaka mine,na umelenga kuwahasisha wanawake kwa asilimia 70 na wanaume kwa asiliamia 30 kujiunga katika vikundi hivyo katika maeneo yao ya vijijini ili kumudu kujikomboa kiuchumi.
Hivyo alisema hamasa watakayoitoa ikiambatana na elimu ya ujasiriamali,itawasaidia wakazi wa vijijini ambako hakuna huduma za Kibenki kumudu kutunza pesa zao kwa kuweka kisha kukopeshana ili kukuza mitaji yao na kuwasaidia kupata maendeleo kwa kasi na wakati.

Aidha Ofisa Mradi huo kutoka Shirika hilo,Fatuma Shaabani,alisema hadi kufikia Julai 2016,wanataraji kuwa wamehamasisha na kusimamia uanzishwaji wa vikundi 291 vyenye jumla ya wanachama 7275.
Ofisa mradi huo alisema watafanikisha jambo hilo kupitia kwa Waelimishaji Ngazi ya Jamii ambao wamewaandaa na kuwapatia elimu ya kutosha juu ya kuhamasisha na kuanzisha vikundi kutoka katika vijiji ambavyo Shirika la HUHESO FOUNDATION limelenga kutekeleza mradi huo.












KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI